Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kuchanganya Maziwa ya mama na vyakula vingine kwa mama mwenye VVU

Kuchanganya Maziwa ya mama na vyakula vingine kwa mama mwenye VVU:

Je,Kwa mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU), kuchanganya maziwa yake na vitu vingine wakati wa Kunyonyesha ni bora kuliko kuacha kabsa kunyonyesha?

Utaratibu wa kawaida kwa mama yoyote: anatakiwa kunyonyesha mtoto kwa miezi 6 maziwa yake pekee bila kumchanganyia mtoto na vyakula vingine, baada ya miezi 6 ndipo aanze kumchanganyia,

Pia licha ya kuanza kumpa mtoto vyakula vingine, anatakiwa kuendelea kunyonyesha mtoto maziwa yake kwa kipindi cha miaka 2 au zaidi akiweza.

SWALI; Je kumchanganyia mtoto vyakula na maziwa ya mama ni bora kwa mama mwenye VVU kuliko kuacha kunyonyesha kabsa?

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO);

Ndyo, Mama anayeishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) anaweza kunyonyesha huku anamchanganyia mtoto na vyakula vingine kuliko kuacha Kabsa kunyonyesha.

Tafiti zinaonyesha kwa mama anayetumia dawa kwa usahihi(ART) hupunguza hatari kwa kiwango kikubwa ya kusambaza maambukizi kutoka kwake kwenda kwa mtoto hata kama mtoto ananyonya na kupewa vyakula vingine,

Ingawa kumnyonyesha mtoto kwa miezi 6 maziwa ya mama pekee pasipo kumchanganyia na vitu vingine hupendekezwa zaidi, kumnyonyesha mtoto pamoja na kumpa vyakula vingine ni bora zaidi kuliko kuacha kabsa Kunyonyesha.

WHO; Yes. Mothers living with HIV can be reassured that ART reduces the risk of post-natal HIV transmission even when the baby is on mixed feeding. Although exclusive breastfeeding is recommended for the first 6 months, mixed feeding is better than no breastfeeding.

KUMBUKA; kuhamanisha wakina mama wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kunyonyesha watoto kwa miezi 6 bila kuchanganya na vyakula vingine bado inashauriwa sana na wataalam wa afya,

Hii ni kwa Sababu ina faida nyingi zaidi, Faida hizo ni pamoja na;

  • Kupunguza hatari ya kupata magonjwa kwa mtoto(maziwa ya mama hutoa kinga bora zaidi)
  • Pamoja na kuboresha ukuaji na maendeleo ya Mtoto

Pia kwa Mujibu wa WHO, Kama mama ni mfanyakazi na anategemea kurudi kazini au ni mwanafunzi, Kuendelea Kunyonyesha mtoto hata kwa muda mfupi ni vizuri zaidi kuliko kuacha kabsa kunyonyesha.

WHO inasititiza kwamba, Ni bora unyonyeshe mtoto hata kwa kipindi kifupi cha chini ya miezi 12 kuliko kuacha kabsa kumnyonyesha mtoto wako.

Mwisho; Ni nini kifanyike kuwasaidia Wakina mama wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kuendelea kunyonyesha watoto wao kama inavyotakiwa?

Ni jukumu la Serikali, Taasisi binafsi,Wadau mbali mbali,Mtu mmoja mmoja,n.k wote kwa pamoja; tuhamasishe na kutengeneza mazingira mazuri ambayo yatamwezesha mama anayeishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) Kuendelea kupata TIBA kama inavyotakiwa(adherent to treatment) pamoja na kunyonyesha watoto kwa usahihi zaidi kwenye mazingira yote ikiwemo;

  • Kwenye jamii
  • Kazini
  • Kwenye vituo vya kijamii
  • Hospital
  • nyumbani n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.