Zaidi ya watu 300,000 wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Morocco
Zaidi ya watu 300,000 wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Morocco:
Zaidi ya watu 300,000 huko Marrakesh na viunga vyake wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Morocco, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) inasema.
OCHA Ilisema: “inafuatilia kwa karibu hali hiyo na iko tayari kuunga mkono juhudi”.
Katika taarifa ya awali, Umoja wa Mataifa ulisema uko tayari “kuisaidia serikali ya Morocco katika juhudi zake za kuwasaidia watu walioathirika”.
Waokoaji wanaendelea kuhangaika kutafuta manusura waliofukiwa na vifusi baada ya tetemeko hilo kubwa la ardhi lililoua zaidi ya watu 2,000.
Credits: BBC