Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa ngiri husababishwa na nini

Ugonjwa wa ngiri husababishwa na nini

UGONJWA WA NGIRI(HERNIA) NINI?,CHANZO,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa Ngiri hujulikana pia kama “Hernia” kwa Kiingereza. Ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni matokeo anayopata mtu kutokana na misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake,

Au kuta hizo kuwa na uwazi na kupelekea viungo hivyo kutoshikiliwa vizuri katika sehemu vinapostahili kuwepo.

CHANZO CHA UGONJWA WA NGIRI

Tunaweza kuufahamu zaidi ugonjwa wa ngiri kama hali inayotokea katika mwili ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu iliyo dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili.

Sehemu inayoathiriwa mara nyingi ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

MAENO AMBAYO HUATHIRIWA NA UGONJWA WA NGIRI

Sehemu ambazo Ngiri inaweza kutokea ni pamoja na maeneo ya:

  • Tumboni
  • Eneo la kinena
  • Eneo la paja kwa juu
  • Eneo ambalo mtu amewahi kufanyiwa upasuaji siku za nyuma
  • Kifuani n.k.

Ugonjwa huu wa ngiri unawapata watu wa jinsia zote na wa umri wowote.

AINA ZA NGIRI AU HERNIA

Aina za Ngiri: Ugonjwa wa mshipa wa ngiri unaweza kujitokeza maeneo mbalimbali ya mwili na aina ya ngiri hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza.

(1) Ngiri maji – Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele)

(2)Ngiri kavu (Hernia) – hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume

(3) Ngiri ya kwenye kifua – hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia

(4) Ngiri ya tumbo – hujulikana pia kama ‘Abdominal Hernia

(5) Ngiri ya kwenye kitovu – hujulikana pia kama ‘Umbilical Hernia”

(6) Ngiri ya sehemu ya haja kubwa – hujulikana pia kama ‘Anal Hernia’

DALILI ZA UGONJWA WA NGIRI-HERNIA

Dalili za aina zote za ngiri hazitofautiani sana na ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote ingawa kuna baadhi ya ngiri hua na maumivu makali kutegemea na jinsi ngiri ilivotokeza.

Ngiri ya kwenye kinena ni ngiri ambayo kitaalamu huitwa inguinal hernia hutokea wakati tishu laini hujitokeza kupitia eneo la udhaifu au kasoro katika misuli yako ya chini ya tumbo. Mara nyingi huwa karibu na eneo la kinena. Mtu yeyote anaweza kupata henia hii, lakini ni kawaida zaidi kwa wanaume kuliko wanawake.

Upasuaji sio lazima kila wakati, lakini henia kwa ujumla inasumbua sana endapo hujafanyiwa upasuaji. Katika baadhi ya matukio, henia isiyotibiwa inaweza kuwa hatari na ya kutishia maisha. Ingawa kuna madhara na hatari zinazohusiana na upasuaji, watu wengi wana matokeo mazuri.

Nini husababisha ngiri ya kinena? Sababu ya ngiri ya kinena haijulikani, lakini inaweza kuwa ni matokeo ya maeneo dhaifu katika ukuta wa tumbo. Ulegevu unaweza kuwa kutokana na kasoro zilizopo wakati wa kuzaliwa au mwili kuingiliwa na sumu baadaye katika maisha.

Baadhi ya sababu za hatari kwa henia ya kinenani ni pamoja na: 

Watu wazima na watoto wanaweza kupata henia ya kinena, Wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata henia ya kinena, Watu wenye historia ya ngiri wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuwa na ngiri nyingine pia. Ngiri ya pili hutokea kwa upande mwingine.

Je! ni zipi dalili za henia ya kinena? Dalili za ngiri ya kwenye kinena zinajumuisha 

maumivu au, shinikizo, hasa wakati wa kuinua kitu, au kukohoa. Dalili hizi kawaida hupungua wakati wa kupumzika. Wanaume pia wanaweza kuwa na uvimbe katika eneo la ngiri.

Huwezi kutambua dalili yoyote ikiwa hernia yako ni ngumu na ndogo.

MATIBABU YA UGONJWA WA HERNIA

Je, unahitaji upasuaji? Kwa kawaida upasuaji haupendekezwi kama henia haijasababisha tatizo. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba wagonjwa wengi hutibiwa kwa upasuaji, wachache sana hupona kwa dawa.

Daktari wako anaweza kupendekeza upasuaji kama:

  • hernia yako inakuwa kubwa
  • Husababisha maumivu yanayoendelea au kuongezeka
  • Hukusababisha kushindwa kufanya shughuli za kila siku n.k

Hernia inaweza kuwa hatari sana ikiwa  sehemu ya utumbo wako umetoka au kuguswa. Ikiwa hii itatokea, unaweza kuwa na: ·

  • Homa
  •  Kiwango cha mapigo ya moyo kilichoongezeka
  • Maumivu
  • Kichefuchefu
  •  Kutapika
  •  Uvimbe
  •  kuona giza n.k

Ikiwa una dalili hizi au  yoyote kati ya hizi wasiliana na daktari wako mara moja. Hii ni hali inayohatarisha maisha inayohitaji upasuaji wa dharura.

Je, ngiri huathiri nguvu za kiume?

Kama ngiri bado ni ndogo Haiwezi kuathiri chochote katika nguvu za kiume. Hata hivyo, henia ambayo imeshakuwa kubwa inaweza kuathiri nguvu za kiume,

– Ngiri huweza kuathiri kazi ya utaratibu na hali ya utengenezaji wa homoni ikiwemo za kiume(Testosterone). Ukosefu wa testosterone homoni unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Upasuaji mbaya wa ngiri unaweza pia kusababisha shida katika korodani, na kufanya uwezekano wa homoni ya testosterone kutengenezwa kuwa chini.

Hata hivyo, kwa sababu watu wengi wana korodani mbili, hata kama moja inaweza kuwa na shida, nyingine inaweza kuzalisha viwango vya kutosha vya homoni. Ngiri pia huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kuharibu mishipa ya neva iliyo kwenye uume.

Kumbuka; Yapo pia MATIBABU ya kutumia  dawa za asili na mbadala za kutibu matatizo ya ngiri aina zote bila kupasua. Lakini changamoto yake nikupata tiba sahihi,maana sio kila dawa za asili hutibu ugonjwa huu wa Ngiri.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.