Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Saidia Unyonyeshaji Wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku

Ikumbukwe kuwa wiki ya unyonyeshaji ilianza Jana Agosti 1 na kutarajiwa kuhitimishwa Agosti 7, 2023 ikienda sambamba na kauli mbiu isemayo;

“Saidia Unyonyeshaji Wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku”

Elimu ya Afya ikiwemo elimu ya unyonyeshaji ni muhimu sana kwa Wazazi,

Wiki hii imekuwa wiki ya Elimu na dondoo mbali mbali kuhusu unyonyeshaji,

Kwa kumalizia leo,wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambayo ilianza Tarehe 1 Mpaka Tarehe 7 August, Zingatia haya;

1. Muda sahihi wa kumnyonyesha mtoto, Mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee muda wa miezi sita(6) ya kwanza,

baada ya hapa,ndyo unaweza kuanza kumchanganyia na vitu vingine,

Pia hakikisha unaendelea kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa miaka 2 au zaidi ukiweza hata kama umeanza kumpa na vitu vingine.

2. Fahamu Maziwa ya mama yana virutubisho vya kutosha ikiwa ni pamoja na kutoa kinga ya Kutosha kwa mtoto dhidi ya magonjwa.

3. Tenga muda wa kutosha wa kumnyonyesha mtoto

4. Fanya Usafi wa mwili ikiwemo matiti yako kabla ya kuanza kunyonyesha.

5. Kazi isiwe sababu ya kutokunyonyesha, hakikisha unatenga muda wa kumnyonyesha mtoto hata kama unakuwa bzy na kazi.

#Worldbreastfeeding Week.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.