Serikali ya Ufaransa imetangaza kusitisha msaada wa fedha kwa Taifa la Burkina Faso
Serikali ya Ufaransa imetangaza kusitisha msaada wa fedha kwa ajili ya maendeleo na msaada wa fedha za bajeti kwa Taifa la Burkina Faso mara baada ya Nchi hiyo kutangaza kuunga mkono Mapinduzi yaliyofanyika nchini Niger.
AFP wameripoti kuwa uamuzi wa Ufaransa unakuja baada ya Burkina Faso na Mali kutangaza kuwa zinaunga mkono kitendo cha Wanajeshi kumpindua Rais wa Niger huku zikisema endapo ECOWAS itaivamia Niger ili kumrudisha Rais madarakani basi na wao watatangaza vita na ECOWAS na watapigana kuisaidia Niger.
Msaada wa Ufaransa kwenye maendeleo ya Burkina Faso unakadiriwa kuwa ni USD mil 530 na msaada wa Ufaransa kwenye bajeti ya Burkina Faso kwa mwaka jana ulikuwa ni Euro mil 13.
#MillardAyoUPDATES