Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Somalia: Mapigano makali yaibuka baina ya polisi na kundi la wanamgambo

Kumekuwa na makabiliano makali katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kati ya polisi na kundi la wanamgambo linaloongozwa na mwanajeshi wa zamani.

Polisi wanasema wanamgambo hao walikuwa wakiwaibia raia katika mji huo.

Mapigano hayo yalizuka Ijumaa jioni na kuendelea hadi Jumamosi asubuhi na kusababisha afisa mmoja na wanamgambo wawili kuuawa.

Rais wa Somalia hivi karibuni alitangaza operesheni ya kuimarisha usalama katika mji mkuu.

Mhariri wetu wa kikanda wa Afrika, Will Rossanasema kwa miaka mingi mitaa ya Mogadishu ilikuwa imejaa watu wenye silaha nzito – wengi hawakuwa sehemu ya jeshi la Somalia au jeshi la polisi.

Sauti ya milio ya risasi ilikuwa ya kawaida na wakati mwingine raia waliuawa wakati silaha zilipofyatuliwa ili kuondoa msongamano wa magari. Lakini mambo yanabadilika.

Rais Hassan Sheikh Mohamud amepiga marufuku silaha nzito katika mji huo na anataka kuimarisha usalama.

Wakati polisi jana usiku walipojaribu kuwanyang’anya silaha wanamgambo wakiongozwa na mwanajeshi wa zamani anayejulikana kama Jenerali Sheegow , ufyatuaji risasi huo ulidumu kwa zaidi ya saa kumi.

Msemaji wa polisi amesema operesheni hiyo ilifanikiwa na kiongozi huyo wa wanamgambo alikamatwa pamoja na wapiganaji wake ishirini na wanne.

Chanzo:Bbc

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.