Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tanzania Yaishukuru Who Kwa Kushirikiana Kudhibiti Ugonjwa Wa Marburg

Tanzania Yaishukuru Who Kwa Kushirikiana Kudhibiti Ugonjwa Wa Marburg

Gaborone – Botswana

Serikali kupitia Wizara ya Afya imelishukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa namna lilivyoshirikiana na Tanzania wakati wa kudhibiti janga la ugonjwa wa Marburg na kupelekea ugonjwa huo kudhibitiwa kwa haraka sana na hivyo kuzuia kusambaa maeneo mengine

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakati akichangia mada kwa niaba ya Waziri wa Afya katika mkutano wa WHO kanda ya Afrika unaoendelea Gaborone nchini Botswana.

Aidha, Dkt. Magembe ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha huduma za afya kuanzia ngazi ya Msingi na kupelekekea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, vifo kwa Watoto chini ya miaka mitano. Pia kuiwezesha Tanzania kuwa kati ya nchi tano za mwanzo ambazo zimeweza kufikia malengo ya 95 95 95 ya mapambano dhidi ya UKIMWI.

“Kwa sasa asilimia 96 ya wanaokadiriwa kuishi na VVU wamepima na kutambua hali zao za maambukizi. Kati ya hao asilimia 98 wanatumia dawa za kufubaza VVU na kati ya hao asilima 97 wamefikia kiwango cha kufubaza VVU”. Amesema Dkt. Magembe.

Kutokana na ongezeko la magonjwa ya mlipuko na madhara mengine ya kiafya ikiwemo dharura mbalimbali duniani, Dkt. Magembe amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuwezeshwa kukabiliana na majanga hayo kwa kuimarisha mifumo ya Afya itakayowezesha kuzuia, kutambua mapema na kukabiliana na majanga hayo kuanzia ngazi ya Jamii.

Ili kuwezesha utayari huo, amesisitiza Shirika la Afya Duniani kuangalia suala la kuwa na mfumo wa kisheria katika uzalishaji wa Dawa na Chanjo, Soko la bidhaa za Afya, uhamishaji wa teknolojoa na uendelezaji wa tafiti kupitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili kuleta uwiano kati ya nchi za kiafrika na nchi nyingine jambo litakalorahisisha upatikanaji wa dawa, chanjo, vifaa tiba na bidhaa nyingine za afya kwa urahisi na kwa gharama nafuu wakati wote kutakapo tokea mlipuko wowote

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.