Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ukungu Kuzalisha Maji Wilaya ya Mbulu

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Comrade Kheri James @comradekheri ameupokea ujumbe wa Taasisi ya Viva con Agua na ENVISOL kutoka Chuo cha Nelson Mandela Arusha ambazo zimekusudia kupeleka huduma ya maji katika Shule tatu za Wilaya ya Mbulu, kupitia mradi wake wa uvunaji wa ukungu.

Akiongea na DC wa Mbulu pamoja na Wataalamu wa Mamlaka za Maji katika Wilaya ya Mbulu, Kiongozi na Mratibu wa Mradi huo Profesa Karoli Njau, amesema Wilaya ya Mbulu ni miongoni mwa Wilaya zenye utajiri mkubwa wa ukungu hivyo wameona ni vizuri na busara kutumia ukungu huo kama fursa ya kupunguza tatizo la maji katika maeneo ya huduma yalio mbali na huduma ya maji lakini yenye utajiri wa ukungu.

Mradi huu hauna mashariti yoyote kwa Shule zitakazonufaika, isipokuwa kigezo kikuu ni Shule hiyo iwe eneo lenye ukungu wa kutosha na ambalo halina huduma kabisa ya maji, mradi utaanza mapema mwezi ujao na utaanza kwa kuwajengea uwezo na uelewa Viongozi na Watumishi wa maeneo yote yatakayonufaika na mradi huo.

Shule zitakazo mnufaika na mradi huo ambao utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa Matumizi ya kibinaadamu na kitaaluma ni Shule ya Sekondari Nambis na Shule ya Msingi Haysali zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, na Shule ya Msingi Hayseng iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.