Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kuanzia Leo tarehe 21:utoaji chanjo ya Polio ya Matone kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 8 katika Mikoa sita (6)

Leo tarehe 21 hadi 24 Septemba, 2023 Serikali kupitia @wizara_afyatz na @ortamisemitz inaendesha zoezi la utoaji chanjo ya Polio ya Matone kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 8 katika Mikoa sita (6) inayopakana na nchi zenye mlipuko wa Polio ambayo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.

Kupitia zoezi hili tunatarajia kuwafikia watoto 3,250,598 waliozaliwa baada ya mwaka 2016. Chanjo hi ya matone (nOPV2) inatolewa ili kuwakinga watoto dhidi ya Kirusi cha Polio aina ya pili (Polio Virus Type 2) kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu.

Tumeandaa timu za watoa huduma za afya za watu watatu watatu ambapo zina jumla ya watoa huduma 5,291 waliopo kwenye Mikoa yote sita (6) inayolengwa.

Nitoe rai kwa wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watoa huduma za afya ili kuwezesha watoto wote walengwa kupata Chanjo hii.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.