Maadhimisho Ya Siku Ya Kuzuia Kujiua Duniani Septemba 10,2023
Maadhimisho Ya Siku Ya Kuzuia Kujiua Duniani Septemba 10,2023.
Katika siku za hivi karibuni pamekuwa na ongezeko la watu wenye msongo wa mawazo ,woga, wasiwasi, kote ulimwenguni.
Unyanyasaji wa Kijinsia katika jamii, mitindo na changamoto za kukabiliana na maisha zinachangia sana kuathiri Afya ya akili kwa watu wengi na kupelekea kujiingiza katika matumizi ya vilevi kupita kiasi,kukata tamaa ya kuishi, hisia za kutaka kujiumiza.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani(WHO), watu 3000 hujiua Kila siku duniani.
Ili kukabiliana na changamoto hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Kuzuia Kujiua kila ifikapo Septemba 10 kila mwaka.
Lengo la Maadhimisho haya ni kuongeza Elimu na uelewa kwa Jamii kuhusu Kinga juu ya Matukio ya kujiua na kupunguza unyanyapaa kwa Jamii ya watu walioathirika.