Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Makubaliano ya ulinzi kati ya Marekani na Kenya yameshasainiwa tayari

Marekani na Kenya zimesaini makubaliano ya ulinzi ambayo yataifanya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupata vifaa na msaada mwingine kwa ajili ya ajili ya shughuli za kijeshi.

Chini ya makubaliano hayo, Kenya itaongoza ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani nchini Haiti utakaokuwa na jukumu la kupambana na magenge yanayosababisha machafuko nchini humo.

Makubaliano hayo ya ulinzi kati ya Marekani na Kenya yalisainiwa jana Jumatatu kati ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, na mwenzake wa Kenya, Aden Duale, katika mkutano uliofanyika jijini Nairobi.

Austin amesema serikali ya nchi yake itashirikiana na bunge kupata dola millioni 100 kwa ajli ya shughuli za kijeshi za kulinda amani nchini Haiti.

Makubaliano hayo ya Marekani na Kenya yatatowa mwelekeo wa sera ya ulinzi katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa kipindi cha miaka mitano, wakati vita dhidi yakundi la al-Shabaab linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida katika eneo la Afrika Mashariki vikiongezeka.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.