Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Malori 5,500 yaliyokuwa yamekwama katika foleni mpaka wa Tanzania na Zambia yapita

Malori 5,500 yaliyokuwa yamekwama katika foleni mpaka wa Tanzania na Zambia wilaya ya Tunduma mkoani Songwe yamefanikiwa kuvuka ndani ya siku kumi.

Kuvuka kwa malori hayo kumesaidia kupunguza msongamano wa magari hayo uliokuwapo ambao ulikuwa ukisababisha kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Nuhu Mgodoka ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa Malori Nyanda za Juu Kusini amesema licha kilichofanyika lakini ni vyema sukuhisho la kudumu likatafutwa.

” Serikali ya Tanzania ni vyena iwe na nia ya dhati na kufanya mazungumzo na serikali ya Zambia ili waweze kutekeleza yale ambayo yanaonekana ni changamoto ya eneo hilo. Ni Muhimu mpaka huu ukafanywa kuwa one stop border,” amesema Mgodoka alipohojiwa na ITV.

Akizunguznia suala hilo, Fadhil Matinya ambaye ni dereva alipongeza hatua hiyo huku akisena alitumia muda mchache kabla ya kuingia upande wa Zambia.

Naye Francis Michael ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe alisema wanaona ipo dalili ya kupata suluhisho la kudumu hasa kupitia mkutano wa wakuu wa nchi watakapokutana siku za hivi karibuni.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.