Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watoto 95,455 Kupatiwa Chanjo ya Polio Kyerwa- Kagera

Katika kuelekea kwenye kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 katika mikoa sita nchini timu ya Wizara ya Afya na Mkoa wa Kagera imefika katika ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kuona utayari wa Wilaya ilivyojiandaa na Kampeni ya Chanjo ya Polio inayotegemewa kuanza tarehe 21 hadi 24, Septemba 2023.

Aidha Timu kutoka Wizara ya Afya na Mkoa wa Kagera imefanya kikao na Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya katika Halmashauri (CHMT) katika ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa ambapo wameweza kuona namna wilaya ilivyojipanga na mikakati waliyojiwekea ili kufanikisha zoezi la Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa  Dr. Lewanga Msafiri amesema watoto 95455 watafikiwa ili kupatiwa Chanjo ya Polio katika wilaya hiyo huku wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wakipatiwa mafunzo kwa siku 3 ili kuweza kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu Chanjo ya Polio, Usafi wa mazingira na magonjwa ya mlipuko.

Naye Beauty Mwambebule mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya amesema katika utayari huo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii(WAJA) wakawe mstari wa mbele kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu Chanjo ya Polio kulingana na kuwepo kwa taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa Polio katika nchi Jirani.

Ameongeza kuwa katika kufikia walengwa ni vyema kama Wilaya kuweza kuwashirikisha Walimu wa Afya mashuleni kwani wao wapo karibu sana na wanafunzi ambao ni watoto wenye umri chini ya miaka 8 ili kufanikisha zoezi hilo.

Ikumbukwe kuwa Kampeni ya Matone ya Chanjo inatarajiwa kuanza tarehe 21-24 Septemba, 2023 katika mikoa sita ya Katavi, Kigoma, Mbeya, Songwe, Kagera na Rukwa na itahusisha watoto waliochini ya miaka 8.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.