Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kenya kumtaka Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza kuomba radhi kwa udhalilishaji

Kenya kumtaka Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza kuomba radhi kwa udhalilishaji.

Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya KHRC imemtaka Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza kuiomba radhi Kenya kwa udhalilishaji uliofanywa nchini humo wakati wa ukoloni,

Mfalme Charles na mkewe Camilla wataanza ziara ya siku nne katika taifa hilo la Afrika Mashariki kesho Jumanne, hiyo ikiwa ziara yake ya kwanza kama mfalme katika nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola.

Kulingana na Kasri la Buckingham, Mfalme Charles anatarajiwa kuzungumzia “masuala yaliyoleta uchungu zaidi” katika uhusiani wa kihistoria kati ya Uingereza na Kenya.

Uingereza ilikubali kuwafidia zaidi ya Wakenya elfu 5 waliodhalilishwa na kuteswa wakati wa vita kupigania Uhuru vya Mau Mau, baada ya kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa mahakamani. Uingereza ilikubali kuwalipa fidia ya dola milioni 25.

Source: dw_Swahili

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.