Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mambo kwenye Mtindo wa Maisha ambayo Huongeza Hatari ya Saratani ya Matiti

Mambo kwenye Mtindo wa Maisha ambayo Huongeza Hatari ya Saratani ya Matiti.

Wanawake duniani kote wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani ya matiti kuliko wengine, sababu hizi huongeza hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti;

1. Matumizi ya Pombe,

Kunywa kupita kiasi huongeza viwango vyako vya estrojeni na homoni zingine zinazohusiana na saratani ya matiti.

Inaweza pia kuharibu seli zako za DNA. Ikiwa unakunywa vinywaji vitatu au zaidi vya pombe kwa wiki, hatari yako huongezeka kwa asilimia 15%. Inaongezeka kwa 10% nyingine kwa kila kinywaji zaidi ya vinywaji vitatu vya kila siku. Vinywaji visivyo na ulevi ni mbadala usio na hatari.

2. Uvutaji wa Sigara

Uwezekano wa kupata saratani ya matiti ni mkubwa zaidi ikiwa ulianza kuvuta sigara kabla ya umri wa miaka 17. Baada ya kuacha, hatari yako itabaki juu kwa takribani miaka 20. Ikiwa unahitaji usaidizi wa kuacha, unaweza, hivo tafta msaada wa jinsi ya kuacha mara moja!

3. Vichocheo(Hormones),

Baada ya wanawake wengi kuacha tiba ya uongezwaji wa vichicheo mwilini yaani “hormone replacement therapy (HRT)”mapema miaka ya 2000 kwa ushauri wa wataalamu, viwango vya saratani ya matiti vilishuka miongoni mwa wanawake waliokoma hedhi.

Progesterone na estrojeni kwenye tiba hyo zinazotumiwa wakati wa kukoma hedhi kwa zaidi ya miaka 5 huongeza hatari zaidi ya kupata Saratani ya matiti,

Vidonge vya uzazi  wa mpango vinaweza kufanya vivyo hivyo hasa ukitumia kwa muda mrefu.

4. Mionzi(Radiation),

Tunaweza kupata mionzi mikali kutoka kwenye vyanzo mbali mbali vilivyotuzunguka, mfano kutoka kwenye ardhi,Jua au vifaa kama X-rays,

Baadhi ya tafiti huonyesha kuna uhusiano kati ya mionzi mikali na kupata Saratani ya matiti.

5. Mwanamke kuchelewa sana kuzaa,

Mfano; Mwanamke Mmoja kati ya wanawake 6 wanaoanza kujifungua nchini Marekani kwenye umri wa zaidi ya miaka 35 huwa na hatari kubwa zaidi ya kupata Saratani ya matiti,

Hatari ya kupata saratani ya matiti ni kubwa zaidi ikiwa mimba yako ya kwanza ni baada ya umri wa miaka 30. Hiyo ni kwa sababu unakabiliwa na estrojeni zaidi katika maisha yako yote. Estrojeni husababisha saratani nyingi za matiti kukua.

6. Kutokufanya mazoezi,

Maisha mengi ya kisasa yanajumuisha kukaa. Kukaa tu huongeza hatari ya kupata matatizo kama vile; kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi na saratani ya matiti.

Tafuta njia za kuufanya mwili kuwa active, Simama na tembea wakati wowote unapoweza. Tafuta shughuli ambayo inakuondoa kwenye sofa.

7. Kula mlo usio kamili na Kuwa na kiwango kidogo cha Vitamin D mwilini,

Viwango vya chini vya Vitamin D vinaweza kukuweka katika hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti.

Unaweza kupata vitamin D kwenye vyanzo mbali mbali ikiwemo chakula,

Pata vyakula muhimu kwa afya yako,ikiwemo matunda na mboga za majani, punguza zaidi vyakula vya mafuta mengi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.