Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Rais Biden kuzuru Israel kwa mazungumzo na Netanyahu

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuzuru Israel Jumatano kuthibitisha “kujitolea kwa Marekani” kwa usalama wa Israel. Hayo yakijiri, miito inaongezeka kwa Israel kufungua njia kuruhusu misaada kuingia Gaza.

Israel yaendelea kujiimarisha kijeshi kwenye mpaka wake na Ukanda wa Gaza kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa eneo hilo.

Ziara hiyo ya Rais Joe Biden wa Marekani nchini Israel siku ya Jumatano imetangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken leo Jumanne.

Blinken amesema Rais Biden atathibitisha tena uungwaji mkono thabiti wa Marekani kwa Israel na kujitolea kwa Marekani kwa usalama wa Israel.

Blinken ameongeza kuwa Israel ina haki na wajibu wa kuwalinda raia wake dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi na kuzuia mashambulizi ya siku za usoni.

Akizungumza na waandishi habari, Blinken amesema, amekubaliana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu mpango utakaowezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia ndani ya Gaza.

Blinken aliyerudi Israel baada ya ziara katika baadhi ya mataifa ya Kiarabu kwenye kanda hiyo, alifanya mazungumzo ya zaidi ya saa sita na baraza la mawaziri la vita la Israel, hadi usiku wa manane.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Blinken, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema: “Hivi vitakuwa vita vya muda mrefu; gharama itakuwa kubwa. Lakini tutashinda kwa ajili ya Israeli na Wayahudi na kwa maadili ambayo nchi zote mbili (Israel na Marekani) zinaamini.”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.