Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Rais wa Senegal Macky Sall ameivunja serikali yake ikiwa imesalia miezi michache

Rais wa Senegal Macky Sall ameivunja serikali yake ikiwa imesalia miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, Waziri Mkuu Amadou Ba, ambaye ni mrithi mteule wa Sall kama mgombea urais wa muungano unaotawala, ndiye pekee aliyesalia katika nafasi ya uongozi kwa sasa.

Muundo wa serikali mpya nchini humo unatarajiwa kutangazwa tena hivi karibuni. Baada ya maandamano na ghasia Sall, mwanasiasa wa mrengo wa kati ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, alitangaza kutowania muhula wa tatu ulio na utata.

Wagombea kadhaa wa Urais wanatafuta idadi ya wafuasi inayokubalika kisheria ili kuidhinishwa kuwa wagombea halali.

Hayo yanajiri wakati ambapo mwanasiasa kinara wa upinzani Ousmane Sonko, alishaondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi hiyo, baada ya kuhukumiwa kifungo katika kesi ya unyanyasaji.

Takriban raia milioni 17 wa Senegal wanatarajiwa kumchagua kiongozi mpya wa serikali yao Februari 25 mwakani.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.