Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Watu wanaoishi hadi miaka 100 wana mambo haya yakufanana, Vipimo vya damu vimeonyesha

Watu wanaoishi hadi miaka 100 wana mambo haya yakufanana, Vipimo vya damu vimeonyesha

Utafiti mpya umechunguza kile kinachoweza kuwa cha kipekee kuhusu watu wanaoishi hadi miaka 100 na zaidi.

Waandishi wa utafiti walikuwa wakitafuta tofauti katika utendaji kazi wa mwili kabla ya mtu kuzeeka sana ambao unaweza kupanua uelewa wetu wa kuzeeka na kuishi maisha marefu.

Hii inafanya kuwa utafiti wa kwanza kulinganisha viashirio vya damu vilivyopimwa katika hatua za awali za maisha kwa watu ambao hatimaye waliishi hadi kufikia umri wa miaka mia moja dhidi ya wengine ambao hawakufanya hivyo.

Matokeo yao yanaonyesha kuwa watu waliofikia umri wa miaka mia moja, kwa ujumla, walikuwa na uwezekano wa kuwa na viwango vya chini vya glukosi, kreatini na asidi kwenye mkojo kuliko watu wengine.

Tofauti za wastani kati ya walio na umri wa miaka 100 na wengine zilikuwa ndogo, na watu waliotimiza umri wa miaka 100 walikuwa na thamani mara chache katika sehemu ya chini au ya juu ya masafa yenye afya, wakielekea kubaki katika safu za kati za vipimo.

Watafiti pia waligundua kuwa watu wenye umri wa miaka mia moja walikuwa wametulia katika wasifu wa kimetaboliki na umri wa miaka 65, miaka 35 kabla ya kufikia alama ya karne.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.