Ajiua kisa meseji za mchepuko kwenye simu ya Mumewe
Mwanamke mmoja anayeitwa Marietha Bosco ( 32) Mkazi wa Kijiji cha Marungu Tarafa ya Mpepo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma amefariki dunia baada ya kunywa dawa ya kuulia wadudu chanzo kikiwa ni maumivu aliyoyapata baada ya kusoma meseji za mchepuko kwenye simu ya Mumewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema Marietha alichukua uamuzi huo November 08,2023 baada ya kukuta ujumbe katika simu ya Mumewe wake ambao ulitumwa na Mwanamke mwingine.
“Marietha ameolewa, siku ya tukio Mumewe alienda shambani kwa bahati mbaya au nzuri akaacha simu nyumbani Mwanamke akachukua ile simu akaanza kuipekua kwa kucheki meseji zote za kawaida na za WhatsApp akaona meseji nyingi kati ya Mume wake akichati na Mwanamke mwingine, marehemu akashindwa kuvumilia akachukua dawa ya kuulia wadudu akaikoroga na kunywa akaishiwa nguvu, Majirani walipofika akawaambia amekunywa sumu wakampleka Hospitali lakini akiwa njiani alifariki”