Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Israel yawatambua Watanzania wanaoshikiliwa mateka na Hamas

Serikali ya Israel imethibitisha utambulisho wa watu wawili kutoka Tanzania wanaoaminika kushikiliwa na Hamas tangu shambulio la Oktoba 7 dhidi ya jamii za kusini mwa Israel, karibu na mpaka na Gaza.

Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga walikuwa nchini Israel kama sehemu ya programu ya mafunzo ya kilimo, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel.

“Walitekwa nyara na magaidi wa Hamas na wanazuiliwa mateka huko Gaza,” ujumbe huo ulisema. “Tafadhali ungana nasi kuwaombea warudi salama na mara moja.”

Mollel na Mtenga walikuwa sehemu ya kundi la wanafunzi waliokuwa wakiishi Kibbutz Nahal Oz. Walikuwa wametoweka tangu mashambulizi hayo, lakini Israel ilikuwa bado haijathibitisha utambulisho wao au kuripoti kilichowapata.

Tanzania ilisema Alhamisi kuwa inafahamu kuhusu wanafunzi wawili waliopotea ambao ni sehemu ya kundi la Watanzania 260 nchini Israel, lakini bado haijathibitisha walipo. Watanzania tisa waliokuwa Israel walirejea nyumbani Oktoba 18.

BBC hapo awali ilizungumza na familia ya mmoja wao, Joshua Mollel, ambaye ni mmoja wa mwanafunzi hao lakini ikasema haikuwa imewasiliana naye tangu wakati wa shambulio hilo.

Habari hizo zinakuja huku kukiwa na majadiliano ya pendekezo la Hamas la kuwaachilia mateka. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian, alisema wiki iliyopita kwamba Hamas iko tayari kuwaachilia mateka lakini “ulimwengu unapaswa kuunga mkono kuachiliwa kwa Wapalestina 6,000” ambao wamekuwa wakishikiliwa katika jela za Israel.

“Viongozi wa vuguvugu la ukombozi la Hamas wametangaza kuwa tayari kuwaachilia wafungwa wasiokuwa wanajeshi na Iran, Uturuki na Qatar ziko tayari kutekeleza jukumu lao katika juhudi hii muhimu,” alisema mwanadiplomasia huyo wa Iran.

Ubalozi wa Israel mjini Pretoria awali uliripoti kuwa raia wawili wa Afrika Kusini, raia wa Eritrea na raia mmoja wa Sudan pia walikuwa miongoni mwa waliofariki au kutoweka.

Source:Bbc

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.