Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

MR Ibu muigizaji na mchekeshaji nguli raia wa Nigeria Akatwa Mguu

‘Kufikia saa saba mchana leo(jana), Baba yangu amefanyiwa upasuaji mara 7 hata hivyo ili kuokoa maisha yake na kuongeza uwezekano wake kupona, ilibidi mguu wake mmoja ukatwe.”

“Tukio hili limekuwa gumu kwetu sote lakini imetubidi tukubali ukweli huu mpya wa hali ya baba ili kumuweka hai.”

Mchekeshaji nguli raia wa Nigeria Mr IBU amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji mara 7 na kukatwa mguu wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram familia ya mchekeshaji huyo ambaye jina lake halisi ni John Okafor imewomba Wanigeria wote wamuombee dua mbali na kumchangia fedha za matibabu.

Mr IBU alianza kuugua tangu mwezi Oktoba na ameonekana katika video moja akiwa amelazwa hospitalini, akiomba msaada wa kifedha.

Ugua pole Mr IBU, Je ni filamu gani unaikubali kutoka kwake?

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.