Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Nyama za puani kwa mtoto,chanzo,dalili na Tiba

Nyama za puani kwa mtoto,chanzo,dalili na Tiba

Tatizo la nyama za puani ni tatizo ambalo huweza kuwapata watoto pia, hali ambayo husababisha mtoto kupata shida mbali mbali ikiwemo ya Kupumua.

Dalili za Nyama za puani kwa mtoto

Ikiwa Mtoto wako ana shida ya nyama za puani huweza kuonyesha dalili mbali mbali ikiwemo;

– Kutoa Sauti wakati wa kupumua au mtoto kukoroma(Snoring)

– Kupata shida ya kupumua(kuvuta hewa na kutoa hewa)

– Mtoto kupumua kwa kutumia mdomo badala ya Pua

– Mtoto kuwa na mafua ambayo hayakatiki, ya mara kwa mara

– Mtoto kuvimba pua au kuwa na shida ya Runny nose

– Kupungua kwa uwezo wa kunusa na kusikia harufu ya vitu mbali mbali(Decreased sense of smell)

Mtoto wako anaweza kulalamika kwamba hawezi kunusa na kusikia harufu ya vitu au kuonja chakula na kupata ladha yake, ambayo hii ni athari ya kupungua kwa hisia ya kunusa.

– Pia mtoto anaweza kuonekana kama kuna kitu anajiribu kumeza mara kwa mara, kwa lengo la kusafisha koo na njia ya hewa kwa ujumla,

Na wakati mwingine mtoto anaweza kulalamika kuhisi hali ya muwasho kooni,vidonda n.k

Chanzo cha Nyama za puani kwa mtoto

Sababu halisi ya kusababisha nyama za puani kwa mtoto haijulikani;

“The exact cause of nasal polyps is not known”
Ingawa sababu hizi huongeza hatari ya kupata nyama za puani kwa mtoto;

–  Tatizo la mzio au Allergic rhinitis, ikiwa mtoto anapata shida ya mzio kwa baadhi ya vipindi huweza kupata shida ya nyama puani, kuvimba eneo la pua n.k

–  Tatizo la Cystic fibrosis, ambapo husababisha mucus kwenye mapafu pamoja na viungo vingine vya mwili kuwa nzito kupita kiasi hali ambayo huweza kupelekea maambukizi ya viini vya magonjwa kwa muda mrefu, kupumua kwa shida n.k,

na mara nyingi tatizo hili hugundulika kwa watoto kuanzia miaka 2

– Tatizo la pumu kwa watoto(Asthma), n.k

Matibabu ya Nyama za puani kwa mtoto

Baada ya kuona dalili zozote kama nilivyoorodhesha hapo awali, hakikisha mtoto wako anapata tiba ya tatizo hili la nyama za puani

– Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo la Nyama za Puani

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.