Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la kunyonyoka nywele hujulikana kitaalamu kama alopecia

Tatizo la kunyonyoka nywele hujulikana kitaalamu kama alopecia (tamka ‘’ alopesia’’). Hali hii ya kunyonyoka nywele husabababishwa na mfumo wa kinga ya mwili kushambulia mwili wa mtu husika (autoimmune disorder).

Kwenye alopecia, mfumo wa kinga ya mwili hushambulia mizizi ya nywele (hair follicles) na hivyo kusababisha kunyonyoka kwa nywele.

Wingi wa kunyonyoka nywele hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.Kwa baadhi ya watu, nywele hunyonyoka sehemu ndogo na kusababisha mabaka mabaka madogo ambayo mwanzoni sio rahisi mtu kugundua.Baadae mabaka haya huungana na kuwa sehemu moja kubwa iliyonyonyoka nywele na hatimaye mtu anaweza kugundua.

Kwa wengine, nywele hunyonyoka kwa wingi sana. Baadhi ya wagonjwa wameota  nywele baada ya awali kunyonyoka na kisha nywele hizo hunyonyoka tena. Mara chache hutokea kwa mgonjwa alienyonyoka nywele kuota tena nywele hizo kwa maisha yake yote.

Alopecia haina uhusiano wa umri wala jinsia ya mtu.Kwa hiyo, mtu yoyote anaweza kupata hali hii.

Visababishi vya Kunyonyoka Nywele

  1. Kama nilivyozungumza awali kisababishi cha kwanza ni autoimmune disorder
  2. Historia ya tatizo hili kwenye familia- Petukhova et al, katika utafiti aliofanya mwaka 2010, aliweza kuonyesha kuwa Jeni aina za PRDX5, STX17 pamoja na mabadiliko ya jeni kwenye mnyororo wa 129 single nucleotide polymorphisms yanauhusiano na alopecia areata [1]
  • Historia ya familia ya magonjwa mengine ya autoimmune disorder kama atopy disease, rheumatoid arthritis, celiac disease, ugonjwa wa kisukari (diabetes mellitus type 1 disease) nk
  1. Kichocheo cha mwili aina ya Dihydrotesterone (DHIT)-Husababisha aina ya alopecia ijulikanayo kama androgenic alopecia
  2. Msongo wa mawazo-Telogen Effluvium, kunyonyoka kwa nywele baada ya kupata msongo wa mawazo au baada ya tukio baya maishani (traumatic event)
  3. Utapia mlo (malnutrition)-Ukosefu wa virutubisho aina ya vitamini D, madini chuma,umehusishwa na tatizo hili la alopecia ingawa utafiti zaidi unahitajika katika nyanja hii.
  • Ugonjwa wa tezi la koo (Thyroid disease)

Kwenye androgenic alopecia mwanamume au mwanamke hunyonyoka nywele pamoja na  kupungua kwa mstari wa nywele kwenye paji la uso  na pia nywele hizi huwa kuwa nyembamba.

Kuna aina nne za kunyonyoka nywele kama ifuatavyo;

  1. Alopecia Areata Totalis-Aina hii huonekana sana kwa wagonjwa wa tatizo hili na mgonjwa hunyonyoka nywele zote za kwenye kichwa.Pia aina hii haitabiriki lini itatokea.
  2. Alopecia areata universalis-Ni hali ya kunyonyoka nywele zote kutoka kwenye mwili. Husababisha nywele kutoota tena baada ya awali kunyonyoka. Ikitokea nywele zimeota tena baada ya kunyonyoka, hatimaye nywele hizi zitanyonyoka tena.
  • Diffuse alopecia areata-Kusinyaa au nywele ghafla kuanza kuwa nyembamba (Thinning of hair)
  1. Ophiasis alopecia areata-Kunyonyoka kwa nywele pembezoni na nyuma ya kichwa

Vichagizi vya kunyonyoka nywele ni kama ifuatavyo;

  1. Ugonjwa wa pumu
  2. Down syndrome
  • Upungufu wad amu aina ya Pernicious anemia
  1. Mzio (Allergies)
  2. Vitiligo

Dalili za Kunyonyoka Nywele

  1. Kunyonyoka nywele-Dalili kubwa ya kwanza
  2. Mabaka ya kunyonyoka nywele kwenye kichwa au baadhi ya sehemu za mwili
  • Mabaka huongezeka ukubwa
  1. Kuota kwa nywele sehemu iliyonyoka na wakati huo huo nywele kunyonyoka sehemu nyingine
  2. Kunyonyoka nywele kwa wingi kwa kipindi kifupi
  3. Kunyonyoka kwa nywele kwa wingi wakati wa majira ya baridi
  • Kucha za kwenye vidole vya mikononi na miguuni kuwa nyekundu, zilizochongoka,nyembamba na huvunjika kwa urahisi, ngumu, zenye matundu na zilizopoteza ungaaji wake.
  • Nywele kuwa fupi na nyembamba na kuota ndani na pembezoni mwa mabaka ya nywele (Exclamation mark hairs)
  1. Nywele kuvunjika kabla hazijafika kwenye ngozi (cadaver hairs)
  2. Kuota nywele nyeupe hasa katika sehemu zinazonyonyoka nywele

Vipimo vya Uchunguzi

  1. Vipimo vya damu (Complete blood count)
  2. Biopsy
  3. C-reactive protein test
  4. ESR (Eryhtrocyte sedimentation rate)
  5. Follicle stimulating hormone and Luteinizing hormone tests
  6. Ultrasound ya tezi la koo
  7. Vipimo vya homoni za tezi la koo (Thyroid Function test)
  8. Antinuclear antibody Panel (ANA Test)
  9. Kipimo cha ugonjwa wa kisukari (Blood Glucose test)

Matibabu ya Kunyonyoka Nywele

Hakuna tiba wala kinga ya ya tatizo hili la alopecia.Baadhi ya matibabu yanayotumiwa kupunguza tatizo hili ni;

  • Dawa aina ya corticosteroids za kupaka au sindano
  • Dawa ya ugonjwa wa presha kwenye kundi la antihypertensive vasodilator
  • Topical immunotherapy
  • Gluten free diet kwa wale ambao tatizo lao la kunyonyoka nywele lina uhusiano na ugonjwa wa celiac disease
  • Ultraviolet light therapy-Tiba inayoongeza mzunguko wa damu kwenye mizizi ya nywele na hivyo kuchangia nywele kuota upya
  • Tofacitinib
  • Tiba ya mzio
  • Upandikizaji wa nywele (Hair transplant surgery)

NB: Nywele bado huweza kunyonyoka baada ya kumaliza matibabu haya

Jinsi ya kuishi na tatizo la Kunyonyoka Nywele

  • Punguza msongo wa mawazo
  • Fuata masharti ya daktari kwa wale wenye ugonjwa wa kisukari
  • Vaa wigi, kofia au kitambaa kichwani kama unaona aibu kutokana na tatizo hili
  • Tumia kalamu ya mkaa kuchora nyusi (eyebrow pencil) kwa wale ambao nyusi zao zimenyonyoka
  • Microbalding-Kuchora nyusi
  • Bandika nyusi bandia (Eyelash extensions)

Matibabu ya Tiba Asili

  • Aromatherapy
  • Acupuncture
  • Probiotics
  • Microneedling (vifaa maalum huuzwa mitandaoni sina uhakika kama vinasaidia kupunguza tatizo hili)
  • Virutubisho vya asili (Herbal supplements kama ginseng tea, green tea)
  • Scalp massage (massage ya kichwa)
  • Low level laser therapy
  • Mafuta mbalimbali kama mafuta ya nazi, zaituni,castor oili nk
  • Essential oils kama lavender, rosemary, peppermint, tea tree

NB: Matibabu haya ya tiba asili hayajafanyiwa utafiti wa kitaalamu (clinical trials) hivyo uwezo wake wa kutibu tatizo hili la kunyonyoka nywele haujulikani.Pia sishauri mtu yoyote kutumia tiba hizi asili pasi kufanya utafiti wa kitaalamu. Mara nyingi maelezo ya vifungashio vya tiba asili au wauzaji sio ya kweli na hayana uthibitisho wowote ule.Hata virutubisho kutoka nje yan chi sio vya kuaminika kwani mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani (Food and Drug Administration) hailazimishi watengenezaji wa virutubisho hivi kuhakikisha virutubisho vyao ni salama kwa afya ya mwanadamu.

Marejeo

1.Petukhova L, Duvic M, Hordinsky M, et al. Genome-wide association study in alopecia areata implicates both innate and adaptive immunity. Nature. 466(7302):113-7.2010Natur. 466. PMID 20596022.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.