Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wanyanyua vyuma Vizito wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua ugonjwa wa ngiri (Hernia)

Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mratibu wa kambi ya uchunguzi na upasuaji wa ngiri, Dk Ahmed Binde amewatahadharisha wanaonyanyua vyuma vizito kupindukia kwa lengo la kutengeneza muonekano wa miili yao ‘Body’ kuwa wako hatarini kuugua ugonjwa wa ngiri (Hernia).

Ngiri ni hali inayotokea pindi ukuta wa tumbo unaojengwa na msuli unapopoteza uimara ama kulegea na hivyo kutengeneza maumbile au uvimbe uliopenyeza katika msuli huo.

Mbali na wanaozaliwa na ngiri, Dk Binde ametaja makundi mengine yaliyo hatarini kuugua tatizo hilo kuwa ni wanaume wenye Saratani ya tezi dume, wanaohangaika kupata haja kubwa kwa muda mrefu na wanaonyanyua mizigo mizito.

Akizungumza leo wakati wa kambi maalum ya siku mbili ya upimaji wa magonjwa ikiwemo ngiri, Dk Binde amewataka wanaonyanyua vyuma kwa lengo la kutengeneza muonekano kufanya hivyo kwa kufuata miongozo ya watalaam wa mazoezi ili kuepuka tatizo hilo.

“Sababu kubwa za kupatwa ngiri mojawapo ni wanaonyanyua vitu vizito vikiwemo vyuma (Gym), gym ni sehemu ya afya lakini kubeba uzito kupindukia kwa mhusika kunasababisha kuongeza mgandamizo (Pressure) kubwa katika tumbo na kuathiri ukuta wa misuli ya tumbo lake baadae kusababisha ngiri, pia watu wanaobeba mizigo mizito pia wanaweza kukumbwa na tatizo hili,” amesema Dk Binde

Kuhusu matibabu, Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, Dk Fabian Massaga amesema matibabu pekee ya tatizo hilo ni upasuaji ambapo ametaja upasuaji wa matundu madogo kuwa ndiyo unatumika katika hospitali ya Bugando.

Pia amesema, Ripoti ya Utafiti uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ya mwaka 2018 inaonyesha kati ya watu 100,000 nchini, wanawame 60 na wanaume 350 wana tatizo la ngiri hivyo akawataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupima tatizo la ngiri.

Kwa upande wake, Mkazi wa Nyamhongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Rehema Kwema ameeleza kushtushwa na taarifa kuwa wanawake wanaugua ngiri huku akitoa wito kwa Bugando kutoa elimu kwa umma kuhusu tatizo hilo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.