Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Akiulizwa anasema alijua litaungua duka moja” RC Albert Chalamila

Uchunguzi wa chanzo cha moto Mwenge, tumebaini kijana mmoja ambaye alichoma duka moja la Nely Mabegi hatimaye moto ukasambaa kwenda maduka mengine na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabishara.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema;

“Chanzo cha moto, duka lilichomwa na binadamu mmoja wa eneo hili. Na hili duka viashiria vinaonyesha mwenye duka aliacha hela, na kuna kijana aliyekuja akafungua duka, akachukua hela na kuchoma moto ili kupoteza ushahidi.

“Jeshi walipomshtua baadhi ya hela akazitupa nyuma pale, ndiyo maana kule nyuma kuna vipande vya shilingi elfu kumi kumi, viko nje kabisa ya maduka, ni hela zilizotoka hapa dukani.

“Jeshi la polisi linaendelea kuchunguza kama kuna mtandao wowote zaidi, ili wote waliohusika watiwe nguvuni na wapate adhabu inayostahili.

“Wakati mwingine mnaweza kudhani ni Serikali au kitu gani lakini ni ninyi kwa nyinyi wafanyabiashara ndiyo mnaleta hasara hizi. Hapa kuna hasara lubwa imetoke kwa sababu ya wizi wa kijana mmoja kufuta ushahidi ili asikamatwe.

“Akiulizwa anasema alijua litaungua duka moja. Kwa hiyo ndugu zangu achene kuweka pesa madukani, hela akiiona kijana wako, hawa vija asio wazuri, atakuja kukutoa roho.

“Nawashukur Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wialaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, nimeona nije nishushe pumzi kwanza. Sio Serikali wala hakuna mtu anayeichukia Serikali kuja kuchoma hapa au jambazi kutoka nje, bali ni sisi kwa sisi ndiyo ambao tumeleta madhara haya, kikulacho kinguoni mwako.

“Jeshgi la Polisi na Zimamoto bado wanaendelea na ufuatiliaji wa kutosha ili kuchukua hatua zinaozstahili kwa wahusika wote mapema iwezekanavyo.

“Kama kuna kibali kinachohusika na ujenzi hapa, toeni vibali ili jengo hili lijengwe lirudi kwenye hali yake. Wananchi endeleeni kutulia wakati Srrikali inafuatilia jambo hili kwa umakini,” amesema Chalamila.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.