Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

DRC: Takriban watu 15 wafariki katika maporomoko ya udongo Bukavu

Katika mji mkuu wa Kivu Kusini, ambako Rais Félix Tshisekedi alifanya mkutano wa kampeni siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kwa kuzingatia uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya udongo na kusomba nyumba kadhaa.

Katika wilaya ya Ndendere, “baba, watoto wake watano na wajukuu wawili” “walilifukiwa na udongo na nyumba yao kuharibiwa”, kufuatia maporomoko ya udongo “karibu usiku wa manane”, Albert Migabo Nyagaza, chifu wa kitongoji, ameliamia shirika la habari la AFP.

“Tulisikia kelele kubwa, kama radi,” anasema Medo Igunzi Munene, mkazi wa eneo hilo na shahidi wa mkasa huo. Anaongeza kuwa aliona “ukuta wa nyumba ukiporomoka kwenye nyingine chini ambapo watu wanane walikuwa wamelala.” Kisha “wakamezwa na udongo”.

Katika vitongoji maarufu vya Bukavu, maporomoko ya udongo, kuanguka na moto wa hatari kumesababisha vifo vya watu kadhaa tangu kuanza kwa mwaka.

Bukavu, ambayo zamani ilikuwa Costermansville iliyanzishwa mwanzoni mwa karne ya 20 kwenye ufuo wa kusini wa Ziwa Kivu na walowezi wa Ubelgiji, iliundwa kwa ajili ya karibu wakaaji 100,000. Leo kuna takriban milioni 2, idadi ambayo ni ngumu kudhibitisha kwa sababu ya ukosefu wa sensa.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.