Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Muswada wa Bima ya Afya kwa wote sasa ni Sheria rasmi

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaini Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.

“Shukrani sana Mhe Rais @SuluhuSamia kwa kujali Afya za wananchi wako husasani wa kipato cha chini na kukubali kusaini muswada wa sheria ya bima ya Afya kwa wote na sasa kuwa sheria kamili.” Amesema Waziri Ummy

Waziri @ummymwalimu amesema kazi iliyombele kwa sasa ni kuhakikisha utekelezaji wa Sheria hiyo inafanyika kwa ufanisi na kwa manufaa ya Watanzania hususani wa kipato cha chini ili kuwawezesha kupata huduma bora za Afya bila ya kikwazo cha pesa.

Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ulipitishwa rasmi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Akson Novemba Mosi, 2023 na kusaini na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Disemba 4, 2023 ili kuwa Sheria.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.