Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na mauaji ya wanawake wawili Wakristo

Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na mauaji ya wanawake wawili Wakristo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na mauaji yaliyoripotiwa ya wanawake wawili Wakristo ambao walikuwa wametafuta hifadhi katika majengo ya kanisa kabla ya kuuawa.

Katika hotuba yake ya kila wiki, kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ameeleza kuwa “raia wasio na ulinzi” wanalengwa kwa kupigwa risasi na kushambuliwa kwa mabomu.

Ameendelea kueleza kuwa, wanawake hao waliuawa na “wadunguaji” na kwamba nyumba ya watawa iliyoanzishwa na Mama Teresa pia iliharibiwa na makombora ya Israel.

Papa Francis pia ametoa wito wa kusitisha mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas uliozuka tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kufanya shambulio ndani ya ardhi ya Israel.

Via:dw

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.