Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

TMA yatoa Tahadhari! Mvua kubwa kunyesha mikoa 7

TMA yatoa Tahadhari! Mvua kubwa kunyesha mikoa 7.

Baadhi ya maeneo katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro na Mtwara yanatarajia kupata mvua juu ya kiwango kwa siku mbili kuanzia leo  Desemba 1, 2023, hivyo wakazi wa maeneo hayo wameombwa kuchukua tahadhari.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa wa siku tano zijazo kuanzia  Novemba 30, 2023 uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliyotolewa Novemba 30, 2023  inaeleza kuwa, mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma inatarajiwa kupata mvua hiyo, Desemba Mosi.

Huku siku siku inayofuata, mikoa ya Morogoro, Ruvuma na Mtwara nayo inatarajiwa kupata mvua hizo.

“Mvua hii itasababisha baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathiri baadhi ya shughuli za kiuchumi.

TMA imekuwa ikitoa taarifa  kila wakati kwa wananchi kuhakikisha hatua muhimu zinafuatwa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.