Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Zahara aagwa rasmi huku utoaji wa heshima za mwisho ukiongozwa na Familia yake

Familia ya mshindi wa tuzo ya uimbaji Zahara, iliongoza utoaji wa heshima za mwisho kwa mwimbaji huyo nyota ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 36.

Albamu yake ya kwanza ya Loliwe ghafla ilimfanya Zahra kuwa na mvuto lakini inasemekana katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akisumbuliwa na tatizo la unywaji pombe.

Zahara alizaliwa Bulelwa Mkutukana, alikuwa amelazwa hospitali tangu mwezi uliopita na familia yake imesema katika taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa Instagram kuwa Zahara alifariki usiku wa Jumatatu “akiwa amezungukwa na familia pamoja na jamaa zake”

“Kipaji kikubwa cha Zahara katika uimbaji na mapenzi aliyekuwanayo kwenye mziki ameyagusa maisha ya mamilioni ya watu” taarifa hiyo iliongeza.

Zahara anajulikana kwa upigaji gitaa wake na mtindo wake wa nywele wa Afro, alizaliwa katika kijiji maskini jirani na East London huko Afrika Kusini.

Alipokuwa mtoto aliimba kwaya na kujifunza kupiga gitaa. Sauti yake ililingamishwa na ya Tracy Chapman, Joan Armatrading na India Arie.

Albamu yake ya kwanza mwaka 2011 iliuzwa ndani ya saa 72 na ghafla ilimbadilisha kuwa mwimbaji nyota wa Afrika.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass