Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Asilimia 40 ya nchi za kipato cha chini zitakuwa maskini zaidi kuliko kabla ya COVID-19

Asilimia 40 ya nchi za kipato cha chini zitakuwa maskini zaidi kuliko kabla ya COVID-19

Benki ya Dunia kupitia ripoti ya matarajio ya uchumi kwa mwaka huu wa 2024 inaeleza kuwa baada ya uchumi wa mwaka 2023 kufanya vibaya, nchi za kipato cha chini zitakua kwa 5.5%, chini ya ilivyotarajiwa na kwamba kufikia mwisho wa 2024, karibu 25% ya nchi zinazoendelea na karibu 40% ya nchi za kipato cha chini zitakuwa maskini kuliko kabla ya janga la COVID-19.

Kwa nchi zenye uchumi wa juu, Benki ya Dunia inatabiri kushuka kwa ukuaji mwaka huu ambao unaweza kutoka asilimia 1.5 za mwaka 2023 hadi asilimia 1.2 mwaka huu 2024.

Mwanauchumi mkuu wa Benki ya Dunia Indermit Gill ameeleza kwamba ukuaji dhaifu wa muda mfupi utasababisha nchi nyingi zinazoendelea, hasa zile maskini zaidi, kufikia “viwango vya juu vya madeni na upatikanaji wa chakula usio wa kuaminika kwa karibu mtu mmoja kati ya watatu.”

“Hilo litazuia maendeleo katika vipaumbele vingi vya kimataifa,” Gill anasisitiza. “Lakini bado kuna fursa za kubadili mkondo,” anangeza, akitoa wito kwa serikali kote duniani kuchukua hatua sasa ili kuharakisha uwekezaji na kuimarisha mifumo ya sera za fedha.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.