Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kasi Yaongezeka sasa kwa Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeongeza kasi ya kutoa elimu na dawakinga kwa jamii ili kuyatokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele ifikapo 2030.

NA: WAF, Dar Es Salaam

Yameelezwa hayo na Afisa Programu kutoka Mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Wizara ya Afya Dkt. Isaac Njau katika semina ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele Duniani (matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho na Minyoo ya tumbo) inayotarajiwa kufanyika Januari 30, mwaka huu.

“Mwaka huu tumejipanga kuadhimisha Siku ya Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, maadhimisho yatafanyika ngazi za mikoa na halmashauri kwa kutoa elimu na hamasa juu ya magonjwa haya katika jamii.” Amesema.

Dkt. Clara Mwansasu ni Afisa kutoka Mpango huo wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa ikitekeleza afua za kutokomeza magonjwa hayo ikiwemo kutoa elimu na kumezesha dawa (NTD’s) baada ya kuwa imefanya tathmini ya kina.

Sambamba na hilo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika utekelezaji wa afua nyinginezo ikiwemo usafi wa mazingira na mwili kwani ni moja ya visababishi vikubwa vya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.