Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Uzazi/Ujauzito

Njia za kuongeza uchungu kwa mjamzito

Njia za kuongeza uchungu kwa mjamzito

Kuongeza uchungu kwa mjamzito, hasa pale ambapo uchungu umesimama au haujaanza kama inavyotarajiwa, ni jambo ambalo linapaswa kufanywa chini ya uangalizi wa kitaalamu wa afya.

Madaktari na wakunga wana mbinu mbalimbali wanazoweza kutumia kulingana na hali ya mama na mtoto.

Hata hivyo, hapa kuna njia zinazojulikana kutumika katika mazingira ya kitaalamu:

1. Matumizi ya Dawa:

Prostaglandins zinaweza kutumika kupitia ukeni ili kuandaa mlango wa kizazi (cervix) kufunguka.

Oxytocin, hormone inaweza kutolewa kwa njia ya drip (IV) ili kuongeza au kuanzisha contractions.

2. Kuvunja chupa ya Maji ya Uzazi(Rapture of membranes):

Mbinu hii, pia inajulikana kama amniotomy, inahusisha kufanya tundu dogo kwenye chupa ya maji ya uzazi. Hii inaweza kusaidia kuongeza uchungu kwa baadhi ya wanawake.

3. Mbinu za Kimwili ikiwemo Mazoezi:

Kuna mbinu za kimwili kama kutembea, kubadili mkao, na kufanya mazoezi maalum yanayoweza kusaidia kuongeza uchungu.

Hata hivyo, mbinu hizi zinapaswa kufanyika kwa ushauri wa daktari au mkunga.

4. Matumizi ya TENS:

Machine ya TENS (Transcutaneous Electrical Nerve Stimulation) inaweza kutumika kutoa stimulation ndogo ya umeme kwenye ngozi, ambayo inaweza kusaidia kupunguza maumivu na kwa baadhi ya kesi, kuchochea uchungu.

5. Acupressure na Acupuncture:

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba acupressure na acupuncture zinaweza kusaidia kuanzisha uchungu, lakini ni muhimu hii ifanyike chini ya uangalizi wa mtaalamu aliyebobea.

NB: Ni muhimu sana kuelewa kwamba njia zozote za kujaribu kuongeza uchungu zinapaswa kufanyika chini ya uangalizi wa kitaalamu.

Kila ujauzito ni wa kipekee, na kuna hatari zinazoweza kujitokeza iwapo mbinu hizi zitatumika bila ushauri na uangalizi wa daktari au mkunga. Kabla ya kujaribu chochote, ni muhimu kujadiliana na wataalamu wa afya wanaofuatilia ujauzito wako.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

#SOMA pia;

Dalili za Mimba changa

Dalili za Uchungu wa kweli

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.