JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA UKIMWI
JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA UKIMWI
Kama ilivyochangamoto kusoma kipimo cha Malaria au Mimba ndivo ilivyo changamoto katika kusoma kipimo cha ukimwi au kipimo cha HIV na kujua majibu sahihi kwa watu wengi.
Huku wengine wakizidi kuchanganyikiwa kuhusu Neno Positive na Negative. Wakishindwa kujua positive ni mtu ambaye ana ukimwi au hana, na Negative ni mtu ambaye ana ukimwi au hana.
Wengine wakisoma majibu yao,wakikuta wataalam wa afya wametumia maneno mbali mbali kama Reactive na Non- reactive.
Katika Makala hii Utajifunza Jinsi ya Kusoma Kipimo cha Ukimwi au Kipimo cha HIV pamoja na baadhi ya maneno ambayo hutumika sana wakati wa Kutoa Majibu;
1. MANENO YANAYOTUMIKA NA MAANA ZAKE
✓ HIV POSITIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi
✓ HIV NEGATIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya Ukimwi
✓ REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi
✓ NON-REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya Ukimwi
2. JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA UKIMWI
– Baada ya kupima kipimo cha ukimwi au Kipimo cha HIV, majibu ya kipimo chetu hutegemea idadi ya mistari itakayojionyesha hapo kwenye Kipimo cha Ukimwi ambapo;
- Kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV kikionyesha Mstari Mmoja, ambapo tunasema mstari wa Control, Aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya ukimwi au ni NEGATIVE au NON-REACTIVE
- Kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV kikionyesha Mstari zaidi ya mmoja kama hapo kwenye picha yetu,Aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi au ni POSITIVE au REACTIVE.
endapo umepima Kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV na mstari wa C-control haujasoma, ujue kabsa umekosea kupima.
FAQs: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, nini maana ya Positive na Negative kwenye kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV?
✓ HIV POSITIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi
✓ HIV NEGATIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya Ukimwi.
Je, ni lazima kipimo cha Ukimwi au kipimo cha Hiv kisome kwenye mstari wa C?
Ndyo,Lazima kipimo cha Ukimwi au Kipimo cha HIV kisome Mstari wa Control-C bila kujali ni Positive au Negative,
Hitimisho
Ni muhimu kufahamu hatua hizi za kupima Kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV ili kupata Majibu sahihi na kuepuka kupata Majibu ya Uongo,
Lakini pia unahitaji kufahamu Zaidi kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi,dalili zake,njia za maambukizi na Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa huu,
• Soma Zaidi hapa:Dalili za Ugonjwa wa UKIMWI
Wakati wa kufanya Kipimo cha Ukimwi au kipimo cha HIV,lazima ujue au Uzingatie mambo haya; kanuni sahihi za Upimaji,Muda wa kusoma majibu yako, expire date ya Kipimo, pamoja na muda wa kurudia vipimo baada ya vipimo vya Awali.
Hello habari ety Kama kipimo kikasoma c n huku kwengn kun mpauko w damu ina maana gani
Vizuri mtaalamu afya za binadamu
Sawa sawa🙏🙏🙏🙏