Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGUMBA WA MWANAUME KUTOKANA NA KUWA NA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME (Low sperm count)

LOW SPERM COUNT

• • • • • •

UGUMBA WA MWANAUME KUTOKANA NA KUWA NA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME (Low sperm count)


Iweje mwanamme wa umri wa kuzaa ashindwe kumpa mimba mkewe?


Inapotokea kuwa mme na mke wanahangaika kupata mtoto, wote wawili wanaweza kuwa ndiyo sababu ya tatizo. Wanaume wanachangia kwa kiwango cha theluthi moja na wanawake pia wanachangia kwa theluthi nyingine moja. Theluthi inayobakia ni matatizo yanayowahusu wote wawili. Kuna mambo mengi ya kuyachunguza, lakini tatizo kuu huwa ni katika mbegu zake mwanamme. 

.

Katika somo letu la leo tutajadili kwa kina mambo ambayo yanaweza kusababisha mbegu za mwanaume zisiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke.

.

UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME


Upungufu wa mbegu za kiume kitaalamu huitwa oligospermia. Hili ni neno linalotumika kuelezea hali ambapo idadi ya mbegu za mwanamme ni ndogo, pungufu ya mbegu milioni 15 katika mililita moja. Kama hakuna mbegu kabisa, hali hiyo huitwa azoospermia. Unapohitaji kupata mtoto, idadi ya mbegu unayotoa wakati wa tendo la ndoa ni muhimu. Idadi ya kawaida ya mbegu ni kati ya milioni 15 hadi milioni 200 kwa mililita moja.


Mbegu zinapomwagwa huwa nzito. Mbegu hizi zinafaa kuchukua dakika kama 20 kabla ya kuwa nyepesi. Kama mbegu zako zinachukua muda mrefu zaidi au zinabaki nzito moja kwa moja, maana yake kuna tatizo.


Unapotazama uwezo wa mbegu kulirutubisha yai, lazima kuchunguza haya yote. Upungufu kidogo katika idadi ya mbegu, kwa mfano, unaweza kusaidiwa na mbegu kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutembea au mbegu kuwa na ujazo mkubwa sana..


DALILI ZA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME. 


Dalili kubwa ya kuwa na upungufu wa mbegu za kiume ni kukosa uwezo wa kumpa mimba mke. Kunaweza kutokea dalili nyingine za wazi. Dalili nyingine zinaweza kuwa:


. Matatizo katika tendo la ndoa – kwa mfano, kukosa hamu ya tendo la ndoa au matatizo ya uume kusimama kwa muda mrefu ili kukamlisha tendo la ndoa.

. Maumivu, uvimbe kwenye maeneo ya korodani

. Kupungua kwa nywele za usoni au za mwilini au ishara nyingine za dosari za homoni.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.