MAUMIVU YA KORODANI
KORODANI
• • • • • •
Maumivu ya korodani ni tatizo linalowasumbua sana wanaume wengi, kawaida maumivu ya korodani hutokea katika korodani moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi.
Maumivu hayo husababishwa na mambo mbalimbali yakiwemo
~ maambukizi ya bacteria au magonjwa ya zinaa
~ kutokunywa maji mengi
~ misuguano inayoathiri moja kwa moja ngozi na mirija ya ndani ya korodani ambayo inaweza kusababishwa na uvaaji wa nguo za ndani zinazobana sana
~ kujikusanya kwa maji na uchafu
~ ngiri
~ Saratani ya korodani au sababu za kupata ajali.
#afya
#jaliafyayako