Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha tatizo la arteriosclerosis,Dalili na Tiba

Chanzo cha tatizo la arteriosclerosis,Dalili na Tiba

Tatizo hili kwa jina la arteriosclerosis, ni tatizo ambalo husababisha maumivu makali kifuani na pia mikono kutetemeka,

Arteriosclerosis  hutokea wakati mishipa ya damu yaani Arteries ambayo hubeba hewa ya Oxygen pamoja na Virutubisho(nutrients) kutoka Moyoni kwenda sehemu zingine za Mwili kuwa thick pamoja na kukakamaa(stiff).

Na wakati mwingine huweza kuzuia hata damu isiende kwenye baadhi ya Viungo pamoja na Tissues,

Kumbuka kwa kawaida Mishipa ya Arteries inatakiwa kuwa flexible na elastic na Sio thick au Stiff.

DALILI ZA TATIZO HILI

Kwa kawaida endapo tatizo lipo kwa kiwango kidogo sana(Mild arteriosclerosis) mgonjwa hapati dalili yoyote ile,

Dalili huanza kujitokeza endapo tatizo ni moderate au severe arteriosclerosis,

Na dalili zake hutegemea na aina ya Mishipa ya Arteries iliyoathiriwa,

mfano;

• Kama tatizo la arteriosclerosis limetokea kwenye mishipa ya arteries ndani ya Moyo, huweza kusababisha maumivu makali ya Kifua,Kifua kuwa kizito,mgandamizo zaidi kifuani,kifua kubana n.k

• Kama tatizo la arteriosclerosis limetokea kwenye mishipa ya arteries inayoelekea kwenye Ubongo,huweza kusababisha tatizo la ganzi,mikono na miguu kuwa dhaifu au kukosa nguvu,mtu kushindwa kuongea, uwezo wa kuona hupotea kwenye jicho moja kwa muda, misuli ya usoni kushuka n.k

• Kama tatizo la arteriosclerosis limetokea kwenye mishipa ya arteries miguuni na mikononi,huweza kusababisha maumivu ya miguu hasa wakati wa kutembea, N.K

CHANZO CHA TATIZO HILI LA ARTERIOSCLEROSIS

Sababu halisi yakutokea kwa shida hii haijulikani, japo huanza na uharibifu au majeraha/kuumia kwa kuta za ndani kwenye mishipa ya arteries, na uharibufu huu huweza kuchangiwa na vitu mbali mbali kama vile;

– Tatizo la Presha kuwa juu

– Kuwa na kiwango kikubwa cha Cholesterol

– Kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu(High triglycerides)

– Uvutaji wa Sigara, tumbaku

– Ugonjwa wa Kisukari

– Shida ya Uzito Mkubwa(Overweight/Obesity)

– Kuvimba, kutokana na magonjwa kama vile arthritis, lupus, psoriasis au inflammatory bowel disease

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA WEWE KUPATA TATIZO LA ARTERIOSCLEROSIS

– Umri kuwa Mkubwa au mtu kuzeeka

– Kuwa na historia ya magonjwa ya moyo kwenye Familia yako

– Kula Mlo wenye madhara kiafya au unhealthy diet

– Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari(Diabetes)

– Kuwa na Tatizo la Presha ya kupanda(High blood pressure)

– Kuwa na kiwango kikubwa cha Lehemu au cholesterol kwenye Damu

– Kutokufanya mazoezi kabsa

– Kuwa na Uzito Mkubwa/Unene n.k

– Uvutaji wa Sigara, tumbaku

– Kuwa na tatizo la kupata shida ya kupumua wakati umelala

– Kuwa na kiwango kikubwa cha Protein aina ya C-reactive protein (CRP), ambayo huwa kama marker ya tatizo la kuvimba au inflammation.

ZINGATIA VITU HIVI;

• Acha kabsa uvutaji wa Sigara au tumbaku

• Kula vyakula ambavyo sio hatarishi kwa afya yako

• Fanya Mazoezi ya Mwili mara kwa mara

• Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa Mwili

• Fanya vipimo vya Presha mara kwa mara,dhibiti Presha yako

• Dhibiti kiwango cha Sukari kwenye Damu,Cholesterol n.k

VIPIMO

– Vipimo vya Damu(Blood tests)

– Electrocardiogram (ECG or EKG)

– Echocardiogram

– Doppler ultrasound

– Cardiac catheterization and angiogram

– Coronary calcium scan n.k

MATIBABU YA TATIZO LA ARTERIOSCLEROSIS

Dawa nyingi hutumika Kudhibiti dalili zinazotokana na tatizo hili,

✓ Statins hizi ni dawa ambazo hutumika kushusha au kupunguza kiwango cha cholesterol,

✓ Aspirin, husaidia kufanya mishipa hii kuwa thin na kuzuia tatizo la blood clots.

✓ Matumizi ya dawa za Presha, Sukari n.k

✓ Na wakati mwingine huduma ya Upasuaji

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.