Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ampiclox inatibu magonjwa gani

Ampiclox inatibu magonjwa gani

Ampiclox ni dawa ambayo inamchanganyiko wa Ampillicin pamoja na Cloxacillin,

COMPOSITION
AMPICLOX CAPSULES.
Each capsule contains Ampicillin Trihydrate BP equivalent to Ampicillin 250mg and Cloxacillin Sodium BP equivalent to Cloxacillin 125mg.

Mchanganyiko huu huifanya dawa ya Ampiclox kuweza kutibu idadi kubwa zaidi ya vimelea vya magonjwa ikiwemo Gram-negative pamoja na Gram-positive bacteria.

Ampiclox inatibu magonjwa gani?

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya magonjwa ambayo dawa ya ampiclox hutibu, na haya ni Majibu ya swali la Ampiclox inatibu magonjwa gani.

Ampiclox capsule inatumika kutibu magonjwa mbali mbali yanayosababishwa na maambukizi ya bacteria(bacterial infections) kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile;

  • Puani
  • Masikioni
  • Kwenye koo
  • Kwenye njia ya hewa
  • Kwenye mapafu
  • Kwenye mifupa n.k

Ampiclox inatibu magonjwa gani

Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo dawa ya ampiclox huweza kutibu;

– Maambukizi kwenye mfumo mzima wa upumuaji au njia ya upumuaji yaani Respiratory tract infections

– Maambukizi kwenye njia ya Mkojo(Urinary tract infection)

– Maambukizi ya bacteria kwenye damu(Septicaemia)

– Maambukizi ya bacteria kwenye Masikio(Otitis media)

– Maambukizi ya bacteria kwenye Pua

– Maambukizi ya bacteria kwenye koo

– Maambukizi ya bacteria kwenye ngozi pamoja na soft tissue

– maambukizi ya bacteria kwenye eneo la moyo(Infective Endocarditis)

– Maambukizi ya bacteria kwenye Mapafu

– maambukizi ya bacteria eneo la nyonga
yaani Pelvic infections

– maambukizi ya bacteria kwenye mifupa-Orthopaedic infections.

Maudhi madogo madogo ya Dawa ya Ampiclox(SIDE EFFECTS):

Side effects za dawa ya ampiclox ni pamoja na;

– Mtu Kuharisha

– Kupata kichefuchefu

– Kupata Maumivu ya kichwa

– Kuwashwa(itching)

– Na wakati mwingine kupata upele kwenye ngozi kwa baadhi ya watu n.k

Usitumie Ampiclox(Contraindications of Ampiclox Capsule)

Kama una allergy na ampicillin, cloxacillin au ingredient zozote za Ampiclox capsule.

KUMBUKA: Kabla ya kutumia dawa hii,hakikisha unapata maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.