Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jitibu magonjwa yote kwa kutumia maji, magonjwa matano ambayo huweza kutibiwa na maji

jitibu magonjwa yote kwa kutumia maji, magonjwa matano ambayo huweza kutibiwa na maji

Katika Makala hii tumeelezea Magonjwa Matano(5) ambayo mtu huweza kupona kwa kunywa maji ya kutosha kila siku.

Inafahamika kwa wengi kwamba mtu anatakiwa kunywa maji lita 2, 2.5 mpaka 3 kwa siku au glass 8 za maji kama kiwango cha wastani cha unywaji maji kwa mtu kila siku,

Ingawa kiwango hiki huweza kuathiriwa na Sababu mbali mbali ikiwemo;

  • Hali ya afya ya mtu kwa ujumla(general body health)
  • Hali ya hewa
  • Kazi anazofanya
  • Mazoezi
  • Umri wake n.k

Magonjwa Matano(5) ambayo mtu huweza kupona kwa kunywa maji ya kutosha kila siku

Aina tofauti za maambukizi ambazo zinaweza kuponywa kwa kunywa maji,

Linapokuja suala la afya yako, maji ni jambo muhimu zaidi, Maji husaidia kuondoa maambukizi na magonjwa mbali mbali.

Hapa kuna baadhi ya magonjwa ya kawaida ambayo yanaweza kuponywa kwa kunywa maji:

1. Ugonjwa wa UTI

Maambukizi kwenye Figo,Njia ya mkojo au kwenye kibofu cha mkojo,

Kama umepata maambukizi ya vimelea kama vile E.Coli, kwenye maeneo haya unashauriwa kunywa maji mengi au yakutosha.

Maji husafisha bakteria walio kwenye kibofu cha mkojo, na hivyo kukabiliana na maambukizi,

Kunywa maji ya kutosha pia huzuia mkusanyiko wa chumvi au madini pamoja na kudilute zaidi mkojo.

Kunywa maji mara kwa mara ni njia nzuri ya kusafisha figo zako na kupona kutokana na maambukizi ya figo,

Walakini, maji ambayo unakunywa hayapaswi kuchafuliwa kwani yanaweza kuzidisha hali hiyo(lazima yawe maji safi na Salama).

2. Ugonjwa wa Fangasi(Yeast Infection)

Ingawa Yapo matibabu mengine ya Fangasi, maji pia huweza kusaidia kama una tatizo la Fangasi, je kivipi?

Yeast hula sukari iliyopo mwilini mwako na kusababisha maambukizi, Lakini Unapokunywa maji ya kutosha, sukari hutolewa kutoka kwa mwili wako na kupunguza sana uwezekano wa mwili wako kuwa na maambukizi mengi ya Yeast.

Hakikisha unakunywa maji safi ambayo hayana sumu ili kuepuka kuongezeka kwa maambukizi ya Yeast.

3. Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji(Respiratory Infections)

Watu wengi hawajui kwamba maji ni msaada mkubwa kwa mtu mwenye maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji ikiwemo magonjwa kama vile asthma n.k

Maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa kupumua ni ya kawaida kabisa, haswa wakati hali ya hewa inapobadilika,

Mtu anayesumbuliwa na maambukizi kwenye mfumo wa kupumua anaweza kupata shida ya kupumua kwa haraka, kutapika, na kuharisha ambayo husababisha kupoteza maji zaidi katika mwili wake.

Kunywa maji katika hali kama hizi ni muhimu sana kwani maambukizi ya kwenye mfumo wa upumuaji husababisha upungufu wa maji mwilini.

4. Shinikizo la juu ya damu(High Blood Pressure-BP)

Maji yana jukumu muhimu katika kudhibiti shinikizo la damu yako. Maji husaidia katika kuifanya damu kuwa nyepesi, na hivyo kufanya iwe rahisi kwa moyo wako kusukuma damu.

Upungufu wa maji mwilini hufanya damu kuwa na asidi, ambayo huongeza viwango vya LDL vya cholesterol,

Kunywa maji husafisha cholesterol iliyozidi mwilini mwako na kuweka njia ya damu safi.

Vyote hivi kwa pamoja husaidia kuweka Sawa Presha yako mwilini.

5. Maumivu ua kichwa(Migraine Headaches)

Ni sahihi kabda kunywa maji mengi huweza kuwa Tiba bora zaidi ya maumivu ya kichwa,

Maji yanaweza kusaidia kupata nafuu kubwa kwa watu wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa au kipandauso.

Ukosefu wa maji mwilini ni kichocheo kikuu cha kipandauso, ndiyo sababu unahitaji kunywa maji mengi,

Watu wanaougua kipandauso wanahitaji kuchukua tahadhari maalum ili kuhakikisha mwili wao unakuwa na maji ya kutosha, kwa kuhakikisha unywaji wa maji mara kwa mara.”

Hayo ndyo Magonjwa Matano(5) ambayo mtu huweza kupona kwa kunywa maji ya kutosha kila siku.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.