Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Unapofikisha miaka 70, kipandauso kilichokuwa kinakutesa kinaweza kutoweka

Unapofikisha miaka 70, kipandauso kilichokuwa kinakutesa kinaweza kutoweka.

Mara tu unapofikisha miaka 70, kipandauso ambacho huenda ulikuwa nacho muda mrefu wa maisha yako kinaweza kutoweka.

Asilimia 10% tu ya wanawake na asilimia 5% tu ya wanaume ndyo huweza kuendelea kuwa na tatizo la kipandauso hata baada ya umri wa miaka 70,

Habari Njema zaidi: Ikiwa una kipandauso, huenda kisije na maumivu ya kichwa. Kadiri watu wanavyozeeka, wengine wanaweza kupata tatizo la kipandauso au migraines kama usumbufu tu au hisia bila maumivu.

Chanzo cha tatizo la kipanda uso(migraine),Dalili na Tiba yake

Kipanda uso au Migraine ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa,

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KIPANDA USO(MIGRAINE)

Maumivu haya makali sana ya kichwa hutokana na sababu mbali mbali kama vile;

hali ya kutanuka kwa mishipa ya damu kichwani kama vile mishipa aina ya Artery,

mabadiliko ya mfumo wa damu yaani Blood stream na mabadiliko ya vichocheo kama vile; kichocheo aina ya Serotonin ambacho huhusika na kudhibiti kiwango cha maumivu kwenye mfumo wa fahamu.

Vyote hivi huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

  •  Mtu kuwa na msongo wa mawazo
  •  Matumizi ya pombe kali kupita kiasi
  •  Kunywa vinywaji vyenye caffeine nyingi kama kahawa N.k
  •  Kukosa muda wa kutosha wa kulala
  •  Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; vidonge vya uzazi wa mpango n.k
  •  mabadiliko ya hali ya hewa mfano; Kuwa na jua kali pamoja na joto sana n.k

DALILI ZA TATIZO LA KIPANDA USO(MIGRAINE) NI PAMOJA NA;

Siku moja au mbili kabla ya tatizo hili kutokea,mtu huweza kupata mabadiliko kama vile;

• Kuanza kupata choo kigumu

• Kupoteza mood

• Shingo kukakamaa

• Kiu ya maji kuongezeka sana pamoja na mtu kukojoa sana

• Mtu kupiga miayo sana

• Kuanza kupata shida ya kutokuona vizuri au kuona marue rue

NDIPO BAADAE dalili zingine hujitokeza mfano;

– Maumivu makali ya kichwa

– Mshipa kucheza cheza  upande mmoja wa kichwani

– Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika

– Mtu kupata kizunguzungu kikali

– Kuhisi sauti za makelele masikioni

– Kupata shida ya kuongea

– Mwili kutetemeka

– Mwili kukosa nguvu

– Dalili za kuchanganyikiwa

N.K

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KIPANDA USO

• Zipo dawa mbali mbali za kuondoa maumivu haya kama vile; Ibuprofen, Paracetum N.k

japo endapo mtu hupata dalili mbaya zaidi kama kushindwa kuongea,mwili kutetemeka, n.k ni vizuri kuwaona wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.