Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kukatika Nywele kwa Wagonjwa wanaopata matibabu ya Saratani #solution

Kukatika Nywele kwa Wagonjwa wanaopata matibabu ya Saratani #solution

Watu wengi ambao hupata matibabu ya saratani huwa na wasiwasi juu ya upotezaji wa nywele au nywele kuanza kunyonyoka/nywele kukatika baada ya kupata matibabu,

Ingawa inaweza kuwa athari ya matibabu fulani ya Saratani, Hali hii haitokei kwa kila mtu anayepata matibabu haya.

Baadhi ya matibabu ya Saratani huweza kusababisha tatizo la nywele kukatika au kutoka kwa kiwango kidogo, hata hivo sio kwa kila mgonjwa anayepata matibabu hayo huweza kupata tatizo hili,

Kwa matibabu hayo hayo, watu wengine hupoteza nywele zao na wengine hawapotezi. Mtoa huduma wako wa afya anaweza kukuambia  kama kuna uwezekano kwa matibabu yako ya saratani kusababisha tatizo la nywele kukatika au la!.

Kwa nini Matibabu ya Saratani yanaweza Kusababisha tatizo la Nywele kukatika?

Dawa nyingi za chemotherapy hushambulia seli zinazokua haraka. Hii ni kwa sababu seli za saratani hugawanyika haraka. Kwa kuwa seli ndani ya nywele au kwenye “hair follicles” pia hukua haraka, dawa za matibabu ya saratani ambazo huenda kwenye seli za saratani mara nyingi hushambulia na seli za nywele kwa wakati mmoja.

Ukiwa kwenye chemotherapy, nywele zako zinaweza kuwa nyembamba, lakini sio zote zitanyonyoka au kukatika. Unaweza pia kupoteza kope zako, nyusi, na nywele za kinena au za maeneo mengine ya mwili.

Kama ilivyo kwa Chemo, mionzi huua seli zinazokua haraka. Wakati chemo inaweza kusababisha tatizo la nywele kukatika kwenye mwili wako wote, mionzi huathiri tu nywele katika eneo linalotibiwa.

Nini kinaweza kutokea?

Tatizo la nywele kukatika mara nyingi hutokea wiki ya kwanza(1) hadi ya tatu(3) baada ya kupata matibabu ya chemotherapy kwa mara ya kwanza au matibabu ya mionzi,

Nywele za kichwa chako zinaweza kutoka kwa makundi. Pengine utaona nywele kwenye brashi yako, wakati unaoga, na kwenye mto wako.

Vidokezo vya Kukabiliana na tatizo la Kukatika kwa Nywele

Ikiwa mtoa huduma wako amekuambia matibabu yanaweza kusababisha tatizo la nywele kukatika, unaweza kukata nywele zako mwenyewe na kuwa fupi kabla ya matibabu yako ya kwanza.

Hii inaweza kufanya tatizo la nywele zako kukatika lisiwe kwa kiwango cha kukushtua. Ikiwa umeamua kunyoa nywele kichwani, tumia mashine ya umeme na uangalie usikate kichwa chako.

Watu wengine hutumia wigi na wengine hufunika vichwa vyao na mitandio au kofia. Watu wengine hawavai chochote kichwani, Hapa chochote unachoamua kufanya ni juu yako.

Kama umeamua kutumia Wigi:

Ikiwa unafikiri ungependa kuvaa wigi, nenda saluni kabla ya nywele zako kuanza kutoka ili waweze kukupa wigi inayofanana na rangi ya nywele zako.

Mtoa huduma wako anaweza kuwa na majina ya saluni zinazotengeneza wigi kwa watu walio na saratani.n.k

Jaribu mitindo tofauti ya wigi ili kuamua unachopenda zaidi.

Mapendekezo mengine:

✓ Kuvaa Vitambaa, kofia, na vilemba ni chaguo nzuri zaidi.

✓ Muulize mtoa huduma wako kama tiba ya “cold cap therapy” inakufaa.

Kwa kutumia tiba hii ya kuvaa kofia ya baridi, ngozi ya kichwa inapozwa. Hii inasababisha follicles za nywele kupumzika, Na matokeo yake, tatizo la nywele kukatika linaweza kuwa dogo zaidi.

✓ Vaa vitu vyenye material laini karibu na ngozi yako.

✓ Siku zenye jua, kumbuka kulinda kichwa chako kwa kuvaa kofia au kitambaa cha kuzuia jua.

✓ Pia Katika hali ya hewa ya baridi, usisahau kuvaa kofia au kitambaa cha kichwani ili kuleta mazingira ya joto kichwani.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.