Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Saratani ya Kongosho ni nini,chanzo,dalili na Tiba yake

Saratani ya kongosho ni nini?

Kongosho ni kiungo kilicho karibu na tumbo na kinafanya kazi ya kudhibiti kiwango cha sukari ndani ya damu. Saratani ya kongosho hutokea kama seli za kongosha zitaanza kukua na kuongezeka kwa haraka bila udhibiti. Aina hii ya kansa inasambaa haraka sana. Kwa kawaida, mgonjwa hufa ndani ya mwaka mmoja baada ya kugunduliwa hata kama imegundulika mapema.

Ni nini huongeza hatari ya saratani ya kongosho?

Mambo yafutayo yanaongeza hatari ya kupata saratani ya kongosho;

1. Kama una historia ya kuvimba kwa kongosho,

2. Kuwa na mwanafamilia ambaye amewahi kupata saratani ya kongosho,

3. Hali kadhaa za kurithi ambazo ni nadra sana na,

4. Matumizi ya tumbaku na  matumizi ya pombe

Ni zipi dalili za saratani ya kongosho?

Mara nyingi haisababishi dalili mpaka ikiwa imesambaa sana. Dalili za saratani ya kongosho iliyosambaa ni pamoja na;

– Kupungua kwa uzito wa mwili bila sababu ya msingi,

– Maumivu ya tumbo au maumivu ya mgongo

– Kuwa na manjano kwenye ngozi na kwenye sehemu nyeupe ya jicho,

– Kupungua kwa hamu ya chakula,

– Sonona.

Kwa sababu dalili hizi zinaweza kusababishwa na magonjwa mengine, unapaswa kumwona daktari kama una wasiwasi. Atapendekeza vipimo ili kutambua sababu ya dalili zako.

Saratani ya kongosho inatambuliwa vipi?

Baadhi ya vipimo vinavyotumika kutambua kama ni saratani ya kongosho ni pamoja na;

  • Computed tomography (CT) scans
  • Ultrasounds,
  • Magnetic resonance imaging (MRI) na
  • Kukata kinyama ili kukipima (biopsy).

Unapokata na kuchukua kipande kidogo cha nyama ya kongosho, sampuli hii inachunguzwa chini ya darubini ili kuona seli za kansa.

Saratani ya kongosho inatibiwa vipi?

Chaguzi za matibabu ni pamoja na upasuaji, tiba mionzi, na tiba kemikali. Unaweza kupewa rufaa ili kuonana na daktari bingwa wa upasuaji au kuonana na daktari bingwa wa saratani au magonjwa mfumo wa chakula. Matibabu yanategemea umri, hali ya afya uliyonayo, unaendelea na aina gani ya matibabu, hatua ya kansa na imesambaa kiasi gani.

Kama daktari bingwa wa upasuaji hawezi kuondoa saratani yote, basi lengo la matibabu linaweza kuwa kuzuia kansa isisambae zaidi. Kama saratani imekwisha sambaa na matibabu hayasaidii, basi daktari anaweza kukusaidia kuweka mipango ya kukusaidia uwe na miasha yasiyo na karaha sana katika kipindi ulichobakiza.

Unawezaje kuzuia saratani ya kongosho?

Hakuna njia ya kuzuia saratani ya kongosho. Baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kupunguza hatari ni pamoja na;

✓ Kuacha kuvuta sigara,

✓ Kuhakikisha uzito unabaki katika kiwango sahihi,

✓ Usinywe pombe kupita kiasi

✓ Kula chakula cha afya.

Vyanzo(Source): medlinePlus

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.