Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Asilimia 75 ya Vioo Kuuzwa nje ya Nchi

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza vioo vya ujenzi cha Sapphire Float Glass kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Rais Samia amesema kiwanda hicho kitazaa viwanda vingine hapo baadae na hata kufikia kutengeneza vioo vya magari.

Ameongeza kuwa asilimia 75 ya bidhaa za vioo zitakazotengenezwa kiwandani hapo zitauzwa nje ya nchi ili kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

Kwa mujibu wa Rais Samia, kiwanda hicho kitaifanya Tanzania kuwa washiriki imara katika Soko Huru la Afrika kwa kupeleka bidhaa zake kwenye soko hilo.

Amewaagiza Viongozi wa mkoa wa Pwani kutumia fedha zitakazopatikana kutokana na uwekezaji huo katika kuboresha huduma kwa Wananchi na sio kuongeza viwango vya kulipana posho.

 

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.