Bwana Harusi na Bibi Harusi waungua moto na kufariki
Watu takribani 100 wamefariki na wengine 150 wamejeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye sherehe ya ndoa katika Wilaya ya Hamdaniya, Jimbo la Nineveh nchini Iraq huku Wanandoa wote wawili (Bwana Harusi na Bibi Harusi nao wakiwa miongoni mwa waliofariki).
Naibu Mkuu wa Kurugenzi ya Afya ya Ninawi, Ahmed Dubardani amethibitisha kuwa Wanandoa hao wamefariki pia huku ikihofiwa kuwa idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.
Idara za Ulinzi kwenye eneo hilo imesema moto huo uliwaka katika ukumbi wa harusi baada ya kurushwa fataki wakati shughuli hiyo ikiendelea.
Taarifa za awali zimesema jengo hilo limejengwa kwa vifaa vya ujenzi vinavyoshika moto kwa haraka, na kusababisha jengo kuanguka muda mfupi baada ya kushika moto.