Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Uzazi/Ujauzito

BAO LA KWANZA HUSABABISHA MIMBA

BAO LA KWANZA HUSABABISHA MIMBA

Kumekuwa na dhana hii ya kwamba Bao la kwanza haliwezi kusababisha Mimba,

Na watu wengi wamekuwa wakihangaika kutafta ukweli juu ya hili, kwa kuliona hilo na kukutana na maswali mengi tumeona tutoe ufafanuzi katika makala hii.

JIBU: kwanza fahamu kwamba Bao la Kwanza huweza kusababisha Mimba kwa asilimia 100%, Na kinachoangaliwa sio bao la kwanza,bali kinachoangaliwa ni uwezo wa mbegu zako kufanya urutubishaji,

Na hapa nitakutajia vitu vichache ambavyo huweza kuangaliwa kwenye uwezo wa mbegu zako kufanya urutubishaji au kuweza kutungisha mimba.

1. Quantity, hapa nazungumzia idadi ya mbegu zinazotoka kwa bao moja au single ejaculation,

Kwa kawaida Mwanaume mwenye uwezo wa kutoa mbegu nyingi kwa bao moja(single ejaculation) angalau Million 15 kwa Milliliter ana uwezo mkubwa wa kutungisha mimba.

Kumbuka tatizo la low sperm count(au mwanaume kuwa na mbegu chache) huchangia kwa asilimia kubwa mwanaume kushindwa kumpa mwanamke mimba,

Wakati mbegu za kiume zinasafiri ili kukutana na yai la mwanamke,mbegu nyingi sana hufia njiani kabla ya kulikuta yai,hivo kama unatoa mbegu chache hata uwezo wa mbegu zako kulifikia yai ni mdogo sana, hali hii huchangia kushindwa kufanya urutubishaji na Mimba ikatokea.

2. Movement, hapa nazungumzia uwezo wa mbegu za kiume kusafiri na kulikuta yai la mwanamke,

Ili yai la mwanamke likutane na mbegu ya kiume kisha kufanya urutubishaji(mimba kutokea) ni lazima mbegu za kiume zisafiri hasa kuelekea kwenye mirija ya uzazi yaani Fallopian tubes ambapo kwa asilimia kubwa urutubishaji huu hutokea hapa kwenye mirija ya uzazi.

Baadhi ya wataalam wa maswala ya uzazi wanasema kama angalau asilimia 40% ya mbegu zako zinaweza kusafiri vizuri basi uwezekano wa kutungisha mimba ni mkubwa.

3. Structure(Morphology), Wengine wanasema shape ya mbegu zako za kiume,

Kwa kawaida mbegu zako za kiume zinatakiwa ziwe na shape ya Oval heads pamoja na Long tails, ili kusaidia kusafiri vizuri pamoja na kufanya kazi ya kulirutubisha yai kwa uharaka zaidi.

ikiwa mbegu zako za kiume hazina shape hii,ni ngumu sana kulirutubisha yai na kusababisha mimba kutokea.

BONUS POINT: ZINGATIA HAYA ILI KUBORESHA MBEGU ZAKO ZA KIUME PAMOJA NA AFYA YA UZAZI KWA UJUMLA

– Hakikisha unakuwa na uzito wa mwili unaotakiwa, kama una tatizo la uzito mkubwa hakikisha unatatua tatizo hili mapema zaidi.

– Hakikisha unakula mlo kamili(Balance diet), yaani unakula chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini kwa kiwango kinachohitajika pia,

epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi,chumvi nyingi sana n.k

– Jikinge na magonjwa yote ya zinaa yaani sexual transimitted diseases-STD’s kama chlamydia,gonorhea,syphilis n.k

– Hakikisha unadhibiti tatizo la msongo wa mawazo kama unalo

– Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili

– Epuka uvutaji wa Sigara na unywaji wa Pombe kupita kiasi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.