Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mwanamke wa Kisumu Aliyetelekezwa na Baba wa Mtoto Baada ya Kujifungua Mapacha: “Haikuwa Rahisi”

Purity Adhiambo hivi majuzi alielezea kisa chake cha kuhuzunisha cha kuachwa na mpenzi wake baada ya kujifungua mapacha,

Binti huyo ambaye alikuwa kwenye uhusiano na mpenzi wake tangu chuo kikuu, alisema maisha yake yalibadilika baada ya mpenzi wake kuondoka kwenda mafunzoni Kiganjo. Alikuwa amemhakikishia kwamba wangeishi pamoja na kulea familia yao baada ya mafunzo yake;

hata hivyo, hatima ilikuwa na mipango mingine kwani Purity alijifungua mapacha. Soma Zaidi hapa…!!!!

Binti mmoja mjini Kisumu nchini Kenya aliyetambulika kwa jina la Purity Adhiambo amejitokeza na kisa cha kuhuzunisha cha kutelekezwa na mpenzi wake baada ya kujifungua mapacha.

Purity alieleza story yake ya Maisha inayojumuisha mapambano na kukata tamaa ndani yake, akitumaini kuongeza ufahamu kuhusu hali yake na kuomba usaidizi katika suala la ajira.

Kulingana na Purity, masaibu yake yalianza mnamo mwaka 2021 alipopata ujauzito wa mpenzi wake wa chuo kikuu. Alimhakikishia kuwa watajenga maisha pamoja baada ya kumaliza mafunzo yake huko Kiganjo.

Hata hivyo, Purity aliambia TUKO.co.ke kwamba hatima ilichukua mkondo mbaya alipojifungua watoto mapacha huku baba yao, Brian Odhiambo, akiwa hayupo kwa mafunzo yake.

Licha ya ahadi zake za awali, tangu wakati huo ametoweka, na kumwacha Purity kubeba jukumu hilo peke yake. “Haikuwa rahisi kwangu tangu kijana huyo akimbie majukumu,” Purity alifichua, sauti yake ikiwa nzito kwa hisia.

“Nimekuwa nikiokoka kwa msaada wa wazazi wangu, lakini naweza kuhisi kwamba wanalemewa na mzigo huo. Maisha yamekuwa magumu sana.”

Mpenzi wa Purity alimblock kwenye simu yake, Purity alisimulia alivyojaribu kuwasiliana na mpenzi wake, na kusema kwamba alipuuza simu zake na hatimaye kumblock. Alionyesha hisia zake za msongo wa mawazo na mfadhaiko kutokana na uzito wa hali aliyojikuta nayo.

Akikabiliana na changamoto za uzazi wa peke yake, Purity anafikia jamii ya Kisumu na nchi kwa ujumla ili kupata usaidizi. Ana Diploma ya Usimamizi wa Chakula na Vinywaji, akionyesha dhamira na elimu yake. Licha ya kuhitimu kwake, yuko tayari kufanya kazi yoyote ambayo itamsaidia kuwapa mahitaji mapacha wake na kulinda maisha yao ya baadaye. “Nilikuwa na mpenzi ambaye alinipa ujauzito tukiwa bado chuoni mwaka wa 2021. .

Alikwenda kwa mafunzo Kiganjo na akaahidi kwamba tutahamia pamoja baada ya mafunzo. Nilijifungua akiwa hayupo, na Mungu alinibariki kwa mapacha,” Purity alieleza.

Mama wa mapacha “Maisha yamekuwa magumu. Ninatoa wito kwa yeyote aliye tayari Kisumu kunipa kazi. Sitakuwa mchaguzi kuhusu kazi, mradi tu inanisaidia kuwahudumia watoto wangu.”

Hadithi ya Purity inaangazia changamoto zinazowakabili akina mama wasio na waume katika jamii, haswa wanapoachwa na wenzi wao.

Ujasiri wake wa kushiriki hadithi yake hadharani unaonyesha azimio lake la kushinda dhiki kwa ajili ya watoto wake. Anapotafuta usaidizi kutoka kwa jamii na nafasi za kazi ili kupata ustawi wa familia yake, simulizi yake hutumika kama ukumbusho wa umuhimu wa huruma na usaidizi wakati wa mahitaji.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.