Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la myofascial trigger points,Myofascial pain syndrome

Tatizo la myofascial trigger points,Myofascial pain syndrome

Myofascial trigger points ni sehemu inayoweza kuwasha kupita kiasi na kusababisha maumivu makali kwenye msuli, kwa kawaida inakuwa ndani ya utepe wa msuli wa kiunzi yaani “taut band of skeletal muscle”

ambayo husababisha maumivu makali inapogandamizwa na inaweza kusababisha characteristic referred pain, motor dysfunction pamoja na autonomic phenomena.

Trigger points au Vichochezi vinaweza kuondolewa kupitia hatua kama vile kutumia spray,mazoezi ikiwemo ya kunyoosha viungo na misuli,massage,dawa n.k,

Kwa mtu mwenye tatizo hili huweza kupata maumivu makali sehemu ya mwili, ambayo ni endelevu na yanayoweza kusababisha kupungua kwa mwendo katika misuli iliyoathiriwa.

Na misuli ambayo huweza kuathiriwa ni pamoja na misuli ya shingoni, mabegani, pamoja na eneo la nyonga(pelvic girdle).

Pia huweza kusababisha Maumivu ya kichwa(tension headache), tatizo la masikio kupiga kelele(tinnitus), mtu kushindwa kutembea, maumivu ya mgongo(low back pain) n.k

Myofascial pain syndrome ni ugonjwa wa maumivu ya muda mrefu. Katika hali hii, shinikizo hutokea kwenye (trigger points) ndani ya misuli yako na kusababisha maumivu katika misuli.

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata maumivu makali kwenye misuli

– Kupata maumivu ambayo hayaishi au endelevu

– Kupata shida ya tender Knot ndani ya misuli

– Kutokulala kutokana na maumivu makali n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI

Trigger point kwenye msuli huweza kutokea baada ya sehemu ya tight muscle fibers kupata jeraha au kutumika kupita kiasi, na ndipo hali ya kuvuta na maumivu hutokea kwenye msuli wote.

Hivo baadhi ya Sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili ni pamoja na;

• Kuumia au kupata jeraha kwenye msuli(Muscle injury), trigger points huweza kutokea kwenye msuli baada ya msuli kuumia au kupata jeraha

• Tatizo la msongo wa mawazo(stress) pamoja na wasiwasi(anxiety), tafiti zinaonyesha watu ambao wanapata stress pamoja na wasiwasi mara kwa mara ni rahisi pia kupata trigger points kwenye misuli. N.k

MADHARA YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

✓ Mtu Kupata maumivu makali kwenye msuli

✓ Mtu kuwa na tatizo la kutokulala au kukosa usingizi

✓ Kupata tatizo la Fibromyalgia n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Matibabu ya tatizo hili huweza kuhusisha njia mbali mbali ikiwemo,matumizi ya dawa za vidonge,sindano(trigger point injection),Kufanya mazoezi n.k

Baadhi ya dawa ambazo huweza kutumika ni pamoja na dawa za maumivu kama vile ibuprofen,naproxen sodium (Aleve) n.k

Dawa jamii ya Antidepressants kama vile amitriptyline ambazo huweza kusaidia kupunguza maumivu na kuleta usingizi,

Dawa jamii ya Sedatives kama vile Clonazepam (Klonopin) ambazo huweza kutibu shida ya wasiwasi(anxiety) pamoja na kutokulala,

Ufanyaji wa mazoezi ni muhimu sana kwa mtu mwenye tatizo hili, ikiwemo mazoezi ya kuvuta viungo yaani stretching exercises, kufanya massage kwenye eneo lililoathiriwa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.