Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MADHARA YA SINDANO KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO(Matumizi ya sindano kwa muda mrefu sio salama kwako)

 SINDANO ZA UZAZI

• • • • •

MADHARA YA SINDANO KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO(Matumizi ya sindano kwa muda mrefu sio salama kwako)


Sindano ni mojawapo ya Njia ya uzazi wa mpango ambayo hutumiwa na wanawake wengi siku hizi, Na wengine huchoma sindano za uzazi wa mpango sio kwasababu wanaelewa sana, ni kwasababu watu wao wa karbu kama vile marafiki au ndugu  hutumia au kuwashawishi nawao watumie.


Wataalam wa afya wanashauri kutochoma sindano zaidi ya tatu au Nne kama umetumia sana Njia hii ya uzazi wa mpango.


MADHARA YA KUTUMIA SINDANO KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO NI PAMOJA NA;


1. Kupatwa na matatizo mbali mbali ya hedhi kama vile;


(i). Kublid damu nyingi sana na kwa muda mrefu mfano; zaidi ya siku 7 mtu ana blid


(ii). Kukaa kwa muda mrefu bila kuona siku zako za hedhi Mfano; kwa zaidi ya miezi miwili, mitatu,sita N.K


(iii). Kupata period ambayo haina mda maalum au yakubadilika badilika


(iv). Kupata damu ya vitone tu hata katikati ya mwezi N.K


2. Kukaa kwa muda mrefu bila kushika mimba,kwa wewe ambaye umeamua kuacha na kutafta mtoto. Hapo ndyo tunasema kwa kitaalam sindano za uzazi wa mpango husababisha Prolong Infertility.


3. Kulainisha mifupa yako ya mwili, na kukuweka katika hatari ya kuvunjika kirahisi zaidi.


4. Kupatwa na maumivu makali ya kichwa ambapo wakati mwingine huambatana na kizunguzungu kikali.

N.K


NB; kumbuka lengo letu ni kupanga uzazi na kupata watoto kwa muda ambayo tunahitaji sisi. Sasa kama umechagua njia ya uzazi wa mpango ambayo baada ya kuacha na kutaka mtoto huwezi kupata mtoto kwa muda unaohitaji wewe,basi hapo haupangi uzazi utakuwa unapangiwa uzazi. 


Hivo ni muhmu kwenda hosptal na kukutana na wataalam wa afya wakuelezee njia salama kwako kulingana na uzazi unaotaka kupanga na sio kwa kufata ushauri wa ndugu, jamaa au rafiki.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.