Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Uzazi/Ujauzito

MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA-mjamzito(INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS)

Maandalizi ya kujifungua kwa mama mjamzito ambapo kwa kitaalam hujulikana kama individual birth preparedness(IBP),

Hapa tunazungumzia vitu vyote ambavyo hutakiwa kufanyika kabla ya mama mjamzito kwenda kujifungua, na lengo kuu ni mama mjamzito asipate shida wakati wa kujifungua,pamoja na kujifungua salama.

MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA-mjamzito(INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS)

– Mama mjamzito anatakiwa ahakikishe amepimwa group lake la damu, na kama ni rhesus factor NEGATIVE mfano; A-,AB-,B-,O- ahakikishe anajiandaa kupata sindano ya Anti-D ujauzito ukiwa na umri wa wiki 28-30 au miezi 7

– Umuhimu wa kupima group la damu kwa mama mjamzito,husaidia sana hata pakitokea emergence ambayo huhitaji mama kuongezewa damu kwa haraka,inakuwa rahisi kufahamu mama mjamzito anatakiwa kupewa damu ya aina gani

– Hakikisha umeandaa vitu kama kadi la kliniki la mama, pamoja na vitu vya kwanza ambavyo huhitajika wakati wa mapokezi na kuviweka sehemu moja au kwenye begi moja

– Maandalizi ya kanga, pamoja na baadhi ya nguo za kuvaa ikiwa ni pamoja na chupi zenye material yanayokausha damu kwa haraka na zinazofunika vizuri

– Andaa beseni lako, pamba, gloves,mpira wa kulalia yaani macknitosh pamoja na cord tie ili hata kama vikikosekana hospitalini,tyr unavyo vitu hivi

– Andaa usafiri wako tayari kabla ya sku ya kwenda kujifungua kufika,na unatakiwa kujua kabsa utajifungua hospitali gani kabla ya uchungu kuanza

– Hakikisha utaribu wa nani atakaa na familia yako wakati upo hospitalini,umeshauweka tayari ili kuepuka mawazo mengi wakati ukiwa hospitalini

– Hakikisha umeweka akiba ya pesa kwa ajili ya vitu ambavyo huweza kujitokeza na kuhitaji pesa kwa wakati huo.

Soma hapa zaidi: VIFAA VYA KUJIFUNGULIA NA MAANDALIZI YOTE YA KUJIFUNGUA

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.