Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Uhusiano kati ya Flagyl na Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Uhusiano kati ya Flagyl na Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy) ni hali ambayo yai la mwanamke hurutubishwa kisha kujishikiza na kuanza kukua nje ya mfuko wa uzazi, mara nyingi hutokea kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes.

Hali hii inahitaji matibabu ya haraka kwani inaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa mfuko wa uzazi,kutokwa na damu nyingi na hata kupoteza maisha,

Flagyl ni dawa inayotumiwa kutibu maambukizi ya bakteria pamoja na Parasite, lakini je! Inaweza kusababisha mimba kutunga nje ya kizazi? Makala hii inajibu swali hilo na inaelezea uhusiano kati ya Flagyl na mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).

Flagyl au Metronidazole ni dawa inayotumika Kutibu maambukizi ya parasites pamoja na bacteria yaani antiprotozoal and antibacterial drug,

Licha ya dawa hii kutumika sana kutibu magonjwa mbali mbali, Usalama wa kutumia dawa hii wakati wa Ujauzito bado ni fumbo kubwa,

Hii imepelekea watu kufanya tafiti mbali mbali kuhusu matumizi ya dawa hii na Usalama wake kwa mjamzito na mtoto aliyetumboni.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha madhara ya kutumia flagyl kwenye Kondo la nyuma yaani placenta pamoja na athari kwenye maendeleo ya mtoto tumboni kwa PANYA mjamzito(placental and fetal development effects in pregnant rats).

Dawa hii ya flagyl au Metronidazole ilitolewa kwa njia ya mdomo ambapo panya mjamzito alipewa dose ya 130 mg/kg kwa siku 7 na siku 14,

Majibu yalionyesha kwamba, kwa kundi la panya ambao walipewa dawa hii kulikuwa na upungufu mkubwa wa sehemu za mtoto kujishikiza yaani implantation sites pamoja na total placental disc area,

Hii inaashiria ongezeko la hatari ya mimba kujishikiza sehemu nyingine tofauti na ndani ya mji wa mimba.

Flagyl, ambayo inajulikana kwa jina la kitaalamu kama metronidazole, ni dawa ya kukabiliana na bakteria pamoja na parasites,

Dawa hii Inatumika kutibu aina mbalimbali za maambukizi, ikiwa ni pamoja na;

  • maambukizi ya njia ya mkojo,
  • matatizo ya ngozi,
  • matatizo ya tumbo,
  • tatizo la amoeba
  • maambukizi ya giardia
  • na hata maambukizi ya bakteria Ukeni.

Hata hivyo, Flagyl ina athari kadhaa ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi au nje ya mji wa mimba(ectopic pregnancy).

Kwa mfano, inaweza kuathiri uzalishaji wa homoni za estrogeni na progesteroni, ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa mimba,

Aidha, Flagyl ina athari kwenye misuli, ambapo inaweza kuathiri kazi ya mirija ya uzazi(fallopian tubes), na matokeo yake kuongeza hatari ya mwanamke kupata tatizo la mimba kutunga nje ya mji wa mimba.

Hata hivyo, inapaswa kutambuliwa kuwa matumizi ya Flagyl peke yake hayasababishi mimba kutunga nje ya kizazi, Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza kusababisha hali hiyo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya uzazi wa mpango usio sahihi, matatizo ya kizazi, na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa,

Ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia Flagyl wakati wa mimba.

Mambo mengine ya kuzingatia

Kwa kuwa mimba kutunga nje ya kizazi au nje ya mji wa mimba ni hali hatari, ni muhimu kuchukua hatua sahihi za matibabu mara moja baada ya kugunduliwa,

Hii inaweza kujumuisha upasuaji ili kuondoa mayai ya uzazi yaliyokua nje ya mfuko wa uzazi au matumizi ya dawa za kupunguza ukuaji wa mimba.

Ili kuzuia hatari ya mimba kutunga Nje ya kizazi, ni muhimu kuchukua hatua za kuzuia maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile bakteria,kuepuka matumizi ya dawa hovio na kufuata mpango mzuri wa uzazi.

Kwa mfano, matumizi ya kondomu na kuepuka ngono zisizo salama ni njia sahihi za kuzuia maambukizi ya bakteria,

Aidha, kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango na kupata matibabu sahihi ya magonjwa ya zinaa ni muhimu katika kuzuia tatizo la mimba kutunga nje ya Kizazi.

Ikiwa una dalili zozote za mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy), ni muhimu kutafuta matibabu ya haraka kutoka kwa wataalam wa afya.

Dalili hizo ni pamoja na;

  1. Kupata maumivu makali kwenye tumbo,
  2. kutokwa damu ukeni,
  3. na hali ya kizunguzungu kikali,

Kwa kuwa mimba kutunga nje ya kizazi ni hali ya hatari, kutafuta matibabu ya haraka kutoka kwa daktari ni muhimu sana ili kuepuka madhara makubwa.

Hitimisho:

Flagyl ni dawa inayotumiwa kutibu maambukizi ya bakteria pamoja na parasites, lakini inaweza kuleta hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).

Kwa hiyo, ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia dawa hii wakati wa mimba,

Aidha, kuzuia maambukizi ya bakteria na kufuata mpango mzuri wa uzazi ni muhimu katika kuzuia tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi.

Kwa hiyo, ikiwa una dalili za mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy), ni muhimu kutafuta matibabu ya haraka kutoka kwa wataalam wa afya ili kuzuia madhara makubwa zaidi kutokea.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.